Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania kurejea Mahakama ya Afrika
Habari Mchanganyiko

Tanzania kurejea Mahakama ya Afrika

Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, iko katika mazungumzo ya kurejea kwenye Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), baada ya kujiondoa Novemba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 7 Machi 2020, jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene, baada ya Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, kuiomba Serikali ibadili uamuzi wake wa kujiondoa AfCHPR.

“Hili tunaendelea kulifanyia kazi, zilikuwepo sababu lakini sababu hizo haziwezi zikabakia za kudumu. Pengine hizo sababu zinaweza zikawa hazina uzito kama ilivyokuwa wakati huo maamuzi yanachukuliwa,” amesema Simbachawene.

Waziri huyo wa Katiba na Sheria, amesema Serikali inafanya mazungumzo na Rais wa AfCHPR, Jaji Iman Aboud, ili kupata muafaka wa suala hilo.

“Mchakato unaendelea ndani ya Serikali na tunaendelea kuzungumza na imekuwa concern kubwa ya Rais wa AfCHPR, jaji iman Aboud ambaye ni Mtanzania na mahakama hii iko Tanzania, inakuwa si vizuri sisi Watanzania tunakuwa hatupo kwenye hili, lakini tupewe muda mchakato unaendelea nina imani muda si mrefu maamuzi yatafikiwa na Serikali,” amesema Simbachawene.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

Wakati huo huo, Simbachawene amesema Serikali itafanya majadiliano na wadau kuhusu maboresho ya mifumo inayoshughulikia haki za binadamu, kisha mapendekezo yatakayotolewa yatawasilishwa kwa viongozi wakuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Wameeleza namna inavyokuwa vigumu kufungua kesi mpaka upate kibali. Hayo yote yakizungumzwa na sisi upande wa Serikali tukajua yanayozungumzwa ni yapi,”

“Mimi nitaitisha kikao cha mawaziri wenzangu, tukae tuzungumze na baadae tuwataarifu viongozi wetu wakuu juu ya maoni yetu na masuala ambayo tunadhani yanaweza yakabadilishwa,” amesema Simbachawene.

Vilevile, Simbachawene amesema Serikali itabaki imara katika kulinda haki za binadamu nchini.
“Kimsingi Tanzania itabakia imara katika kulinda haki za watu na kama mnavyofahamu haki za binadamu ni ajenda pana na kwa hivyo hakuna mtu mmoja anaweza kupima hizo haki za binadamu,” amesema Simbachawene.

Novemba 2020, Serikali ya Tanzania, chini ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, ilijiondoa katika Ibara ya 34 (6) ya mkataba wa AfCHPR, inayoruhusu watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuishtaki Serikali.

Serikali ya Tanzania ilichukua hatua hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa haijaridhishwa na baadhi ya mambo yaliyokuwa yanaendelea katika mahakama hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!