Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania kupeleka gesi Uganda
Habari za Siasa

Tanzania kupeleka gesi Uganda

Kituo cha kupokea gesi asilia cha Kinyerezi, Dar es Salaam
Spread the love

 

WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba amesema Serikali ya Tanzania ameanza mazungumzo ya awali na Serikali ya Uganda kutekeleza mpango wa kupeleka gesi nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Amesema mpango huo ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan aliyewaagiza watalaam wa wizara hiyo kuhakikisha mradi wa kuchataka gesi nyingi iliyopo baharini ili kuisafirisha katika masoko mbalimbali, ufanyike haraka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Novemba, 2021 katika kongamano la biashara kati Tanzania na Uganda, Makamba amesema tayari amezungumza na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda, Dk. Ruth Nankabirwa kuhusu suala hilo.

Amesema mbali na ushirikiano katika bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima hadi Tanga, tayari kuna mradi mwingine mpya wa ujenzi wa bomba lingine la kutoa gesi Tanzania kupeleka Uganda.

Rais Yoweri Museven

“Leo tutaanza mazungumzo ya awali kuhusu suala hilo na kutokana na uongozi wenu na dhamira yenu ya kuimarisha mahusiano kati ya nchi zetu mbili.

“Lakini katika kuhakikisha rasilimali asili zilizopo katika nchi zetu pia zinanufaisha majirani zetu na zinawezesha uchumi wa ukanda huu kukua kwa pamoja, kazi hiyo tutaifanya katika mkutano ambao tutakutana baadae,” amesema.

Aidha, akizungumzia ujenzi wa bomba hilo la gesi, Makamba amesema “Nikuhakikishie kuwa kazi hiyo tumeianza na mazungumzo yanaendelea vizuri na tutafika mahala ambapo ndani ya kipindi kifupi tutatoa taarifa kuhusu maendeleo ya kazi hiyo.

“Ni imani yetu ni kwamba baada ya kukamilika kwa mradi huu ukichanganya na mradi wa bomba la mafuta, ramani ya Afrika mashariki kwenye sekta ya nishati duniani itabadilika,” amesema.

Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema ukitazamani nchi za hizo zimegawanywa kwa mipaka ilichorowa, lakini kwa ramani ya siku zijazo haitakuwa ya mipaka baina ya nchi bali itakuwa ya mistari inayoziunganisha nchi mistari.

“Mistari hiyo ni barabara laini za umeme na mabomba ya nishati, nchi zetu mbili zinachora ramani mpya duniani ya kuziunganisha na kuwezesha wananchi wetu na nchi zetu kuendelea kwa haraka zaidi na kupata manufaa makubwa zaidi,” amesema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!