June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kuongoza mkutano wa OGP

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Spread the love

TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Kanda ya Afrika, unaohusu mpango wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi (Open Government Partnership-OGP). Anaripoti Sarafina Lidwino … (endelea).

Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais-Ikulu, mkutano huo unatarajiwa kufanyika Mei 20 hadi 21 mwaka huu, katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika hapa nchini, lakini ni wa pili kufanyika katika Kanda ya Afrika ambapo uliwahi kufanyika Mombasa, Kenya mwaka 2013.

Taarifa hiyo, imesema mkutano huo unatarajiwa  kuwa na wageni 200 kutoka serikalini, asasi za kiraia na washirika wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua.

Aidha, lengo la mkutano huo ni kuongeza uelewa zaidi juu ya uendeshaji shughuli za kiserikali kwa uwazi, kutoa marejesho kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali na uwazi kwa wananchi juu ya ardhi iliyopimwa.

Pia, kupata uzoefu wa utekelezaji wa OGP kutoka kwa nchi wanachama katika Bara la Afrika na kupata maoni na mtazamo wa Asasi za Kiraia katika usimamizi na utekelezaji wa shughuli za serikali. Kauli mbiu ya mkutano huo ni, “Kuimarisha Utawala Bora unaozingatia uwajibikaji na uwazi”.

error: Content is protected !!