August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kulipa fidia Wakenya

Spread the love

MAHAKAMA ya Afrika imethibitishwa kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa watuhumiwa 10 Raia wa Kenya waliotuhumiwa na Serikali ya Tanzania kufanya mauaji kwa kutumia silaha, anaandika Wolfram Mwalongo.

Akisoma hukumu ya shauri hilo leo Fatsach Orguergouz, Jaji wa Mahakama hiyo amesema, walalamikaji wana haki ya kulipwa fidia.

Amesema, kama watahitaji wawasilishe madai yao mahakamni hapo ndani ya siku 30 ili kuanza kwa kesi ya madai.

Watuhumiwa hao walitiwa hatiani na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kosa la mauaji na ujambazi kwa kutumia silaha uliofanyika katika Bank ya NMB Tawi la Moshi Mei 2004 na kuwekwa rumande kwa miaka 10 bila uchunguzi kukamilika.

Katika malalamiko yao, watuhumiwa hao wanadai kuwa Januari 2006, walikamatwa nchini  Msumbiji na kusafirishwa kwa ndege ya kijeshi na kufunguliwa mashtaka ya mauaji na mashtaka matatu ya wizi kwa kutumia silaha.

Hata hivyo wanataka walipwe fidia na pia  wapatiwe wanasheria kwani  haki zao zinaendelea kukiukwa  ikiwemo  ya  kuchelewa  kusikilizwa  kwa  shauri lao.

Mahakama ya Afrika kuhusu haki za binadamu na za watu iliundwa mwaka 2006 na kuanza kazi zake rasmi mwaka mmoja baadaye.

Hadi kufikia mwishoni mwa Februari 2016, mahakama hiyo imepokea kesi 74, ambapo 25 kati ya hizo zimeshughulikiwa, huku kesi 4 zikipelekwa katika Tume ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu nchini Gambia.

error: Content is protected !!