July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kukabili changamoto za maendeleo

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imejipanga kukabili changamoto zilizojitokeza katika mpango wa kwanza wa maendeleo endelevu (UNDAP 1)2011-15, anaandika Hamisi Mguta.

Hayo yameelezwa leo na Dk. Sifuni Mchoma, Katibu mkuu wizara ya Katiba na Sheria katika uzinduzi wa mpango wapili wa miaka mitano ya kusaidia maendeleo endelevu uliofanyika na Umoja wa mataifa (UN) kushirikiana na taasisi zake mbalimbali chini ya serikali ya awamu ya tano.

Dk. Mchoma amesema, malengo waliyokua wameweka katika mpango wa kwanza yalikua ni mengi sana hivyo yalikua na vigezo vingi kujipima.

Amesema, mpango huo unaotajwa kuwekewa bajeti ya Trilioni 2.8 utajikita katika mambo 12 tu yakiwemo Afya, Elimu, Mazingira pamoja na kujenga mihimili ya uchumi ili kuendelea walipoishia.

Mchoma akiyemuwakilisha Dkt. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa hazina kuwa mgeni rasmi katika mkutano huoamesema “Malengo tuliyojiwekea katika mpango wa kwanza tumegundua yalikua ni mengi, sasa tumeona kupunguza tuache vichache;
“Mpango wa kwanza ulijikita pia kwenye masuala ya Afya, Elimu pamoja na Mazingira ispokua mpango huu tunaendeleza tulipoishia na kuyaendeleza mazuri tuliyofanikiwa,”amesema.

Asilimia nane pekee kutoka katika fedha za Mpango huo zimetajwa kuelekezwa Zanzibar, ili kuweza kufanya muendelezo.

Mpango wa kwanza wa miaka minne ulizinduliwa Juni 2011 ukitajwa kutumia bajeti ya 0.8 Dola za Kimarekani huku Tanzania ikiwa Nchi ya kwanza wakati huo kuanza kutumia mpango wa UNDAP.

Juma Malik Akil, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, amesema mpango wa kwanza umesaidia Sana Zanzibar has a katika Sekta ya Uchumi na zakijamii.

” Tunategemea kupitia mpango huu, kupingana na bajeti ilivyo tutapata kuona mafanikio ya kiuchumi na Kijamii,”amesema.

Nae, Alvaro Rodrigues,Mratibu wa mashirika ya Umija wa Mataifa Tanzania, amesema mpango huo unamtaka mtanzania kufanya kazi na kutekeleza wajibu wake Kama ilivyoelezwa katika malengo ya Dunia.

Mkutano huo uliudhuliwa na maofisa wa serikali, viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifana Wafanyakazi wake.

 

error: Content is protected !!