May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kuingiza timu nne michuano ijayo CAF

Spread the love

 

MARA baada ya klabu ya ASC Jaraaf ya Senegal kuondolewa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Coton Sports ya Cameroon ni rasmi sasa Tanzania itaingia timu nne kwenye michuano ya kimataifa kuanzia msimu ujao wa 2021/22 licha ya Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF) kutotoa taarifa rasmi.

Kwenye mchezo huo ASC Jaaf ilibuka na ushindi wa mabao 2-1, na kutolewa kwa faida ya bao la ugenini mara baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0, kwenye mchezo wa kwanza.

Clatous Chama, kiungo wa klabu ya Simba

 Kuingiza timu nne kwa Tanzania kwenye michuano hiyo kumetokana na kuwa na pointi nyingi ukilinganisha timu za Senegal ambayo imetolewa kwenye michuano hiyo ya kimtaifa na kusalia na pointi 15.

Kwa sasa Tanzania ina pointi 27.5 katika orodha ya Shirikisho la mpira wa Miguu Barani Afrika huku Cameroon ikiwa na pointi 11 mara baada ya Coton Sport kuiondoa ASC Jaraaf.

Mukoko Tonombe mchezaji wa klabu ya Yanga

Tanzania imejiongezea pointi hizo kufuatia kufanya viuzri kwa klabu ya Simba kwenye michuano ya klabu bingwa kwenye msimu huu kwa kufika hatua ya robo fainali na kuondolewa na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-3.

Kwa Habari zaidi soma Gazeti la Raia Mwema

error: Content is protected !!