Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tanzania kuingiza aina tano chanjo za Korona
AfyaTangulizi

Tanzania kuingiza aina tano chanjo za Korona

Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inatarajia kuingiza aina tano za chanjo ya Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19), ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo kwa wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 28 Julai 2021 na Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, akizungumza katika uzinduzi wa chanjo ya UVIKO-19, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo wa afya ametaja chanjo hizo kuwa, ni Moderna, Pfizer-BioNtech, Johnson &Johnson, Sinopharm na Sinovac.

Dk. Gwajima amesema, Serikali imeamua kuleta aina nyingi za chanjo, ili kila mwananchi apatiwe chanjo inayoendana na afya yake.

“Hakuna dawa isiyokuwa na mashara lakini kuna faida zake, ndiyo dawa ziko hivyo na jinsi ya ku-manage na daktari kukuona wewe nisikupe hii, nikupe mbadala,” amesema Dk. Gwajima na kuongeza:

“Ndiyo maana chanjo zitakuja nyingi, aina tano ili wananchi wafanye maamuzi, wazisome tuone huyu ana-fit hapa.”

Tarehe 24 Julai 2021, Serikali ya Tanzania ilipokea dozi 1,058,400 za chanjo ya Korona , kutoka katika Serikali ya Marekani, kupitia mpango wake wa Covax. Unaolenga kusaidia nchi zinazoendelea katika kukabiliana na janga hilo. Chanjo hizo ni aina ya Johnson & Johnson.

Leo Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuchanjwa chanjo hiyo, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!