July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kuadhimisha Tabaka la Ozoni

Spread the love

SEREKALI ya Tanzania inatarajiwa kuungana na Jumuiya za Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni litakalofanyika Septemba 16 mwaka huu, Anaandika Faki Sosi…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Rais-Mazingira, Mhandisi Dk. Binilith Mahenge amesema kuwa, Tanzamia itaungana na jumiya hiyo kwenye maadhimisho ya azimio la Umoja wa Mataifa la 49/114 Desemba,19,1994.

Dk. Mahenge amesema kuwa, tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomong’onyoa Tabaka Hewa la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka hilo.

Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya asilimia 98 ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa tabaka hilo.

Dk. Mahenge amesema kuwa, 1996 serikali iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni.

Mikakati hiyo ni pamoja na kujenga uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa mkataba, kuweka takwimu za kemikali hizo, kutoa elimu kwa wadau na kwa umma kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili, kusambaza habari kuhusu kemikali na teknolojia mbadala na mikakati mingineyo.

“Hatua hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na mkataba na tumeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86 ya kiasi cha matumizi ya kemikali hizo, mwaka 1999,” amesema Dk. Mahenge.

Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipodozi (Refrigerant Management Plan). Katika utekelezaji wake, mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo kuandaa Kanuni za Usimamizi wa Kemikali zinazomong’onyoa tabaka hilo ambazo zilianza kutumika Desemba 7, 2007.

Pia, kusambaza kwa vitambuzi vya kemikali hizo vipatavyo 18 kwa ajili ya vituo vilivyo mipakani mwa Tanzania, pia kusambaza mitambo na zana za kuhudumia majokofu na viyoyozi kama vile mashine za kunasa na kurejeleza gesi chakavu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya fani ya kuhudumia majokofu na viyoyozi hapa nchini.

Dk. Mahenge amesema, kwa hapa nchini maadhimisho haya yatafanyika kwa njia ya uelimishaji umma kuhusu Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa tabaka hilo na matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa Tabaka la Ozone.

error: Content is protected !!