January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kinara watoto wenye utapiamlo

Mtoto mwenye Utapiamlo

Spread the love

SERIKALI imekiri kwamba Tanzania ni nchi ya tatu katika Bara la Afrika kwa kuwa na watoto wengi wenye utapia mlo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Kebwe Steven Kebwe, alipokuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassm Ahamed (CCM).

Katika swali la msingi la mbunge huyo,alitaka kujua serikali inachukua hatua gani mahususi za kuhakikisha inapambana na tatizo hilo.

“Tanzania inachukua nafasi ya tatu Barani Afrika kuwa na watoto wanaodumaa kiakili.

“Je, serikali inachukua hatua gani mahususi za kuhakikisha inapambana na tatizo hilo”alihoji mbunge.

Akijibu swali hilo Kebwe amesema tatizo la watoto kudumaa kiakili lipo katika nchi nyingi duniani na linatokana na ulaji duni wa vyakula vyenye virutubisho vya kutosha.

Jumla ya watoto milioni 199 sawa na asilimia 33 duniani wa chini ya miaka mitano walikuwa wamedumaa kufikia mwaka 2000.

Amesema juhudi zinafanyika kupunguza tatizo hilo hadi kufikia watoto milioni 161 sawa na asilimia 25 kwa mwaka 2013.

Dk. Kebwe amesema kutokana na utafiti wa Kidemografia wa Afya wa mwaka 2010 asilimia 42 ya watoto chini ya miaka mitano walionekana kuwa na udumavu kwa maana ya urefu wao kutolingana umri wao.

Mbali na hilo Dk. Kebwe amesema njia pekee ya kuondokana na tatizo la utapiamlo ni wazazi kupata elimu ya kuwapatia lishe watoto wao.

Mbali na hilo amesema ni muhimu mama kumnyonyesha mtoto wake kwa muda wa miezi sita bila kumpatia chakula kingine.

Alieleza kwamba kwa sasa serikali inaendelea na utoaji wa elimu kwa jamii ili kuhakikisha watoto wanapatiwa lishe bora.

“Iwapo jamii itapata elimu inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuwapatia lishe bora watoto waliopo chini ya miaka mitano ni wazi kuwa tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa” amesema.

error: Content is protected !!