Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tanzania ipo tayari kuilisha Dunia
Habari Mchanganyiko

Tanzania ipo tayari kuilisha Dunia

Mahindi yakiwa shambani
Spread the love

 

KWA mujibu wa takwimu kutoka Benki ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Kilimo, Tanzania imeongeza mauzo ya nje ya chakula mwaka hadi mwaka, huku chakula hicho kikiuzwa nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Pembe ya Afrika (Horn of Africa) na sehemu nyingine mbalimbali duniani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania iliucha mboga mboga zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.01 (Shilingi trilioni 2.4) katika kipindi cha miaka mitano kati ya mwaka 2018 hadi 2022.

Tanzania pia iliuza mazao ya nafaka (zaidi mchele na mahindi) yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 999 (Shilingi trilioni 2.3) katika kipindi hicho cha miaka mitano iliyopita.

Mauzo ya nje ya nchi ya samaki na bidhaa za samaki yalifikia Dola za Marekani milioni 800 (Shilingi trilioni 1.9), wakati matunda yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 71.4 (Shilingi Bilioni 170) kati ya 2018 na 2022.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa watano wa mchele kwenye bara zima la Afrika na ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa mchele Afrika Mashariki.

Katika msimu wa 2020/21, Tanzania ilizalisha tani milioni 1.85 za mchele, wakati mahitaji ya nchi kwa mwaka ni takribani tani milioni 1. Maana yake ni kuwa mchele wa ziada ulikua tani 850,000.

l

Katika msimu huo huo, Tanzania ilizalisha tani milioni 6.5 za mahindi, ukilinganisha na nahitaji ya taifa ya tani milioni 6 kwa mwaka.

Takwimu hizi zinaibuka huku Rais Samia Suluhu Hassan leo akizindua maandalizi ya mkutano mkubwa wa Kilimo wa Afrika (Africa Food Systems Forum) ambao unatarajiwa kufanyika Tanzania Septemba 5-8, mwaka huu.

Uzinduzi huo umefanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Tangu aingie madarakani mwezi Machi 2021, Rais Samia ameongeza bajeti ya serikali kwenye kilimo maradufu kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Serikali ya Samia imewekeza kwenye ruzuku ya mgbegu, ruzuku ya mbolea, uzalishaji mbegu na kilimo cha umwagiliaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!