Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania inakabiliwa na uhaba wa nyumba milioni 3
Habari Mchanganyiko

Tanzania inakabiliwa na uhaba wa nyumba milioni 3

Spread the love

 

TANZANIA inakabiliwa na uhaba wa nyumba zipatazo milioni tatu licha ya kuwa watanzania ni zaidi ya milioni sitini ambapo jiji la Dar es salaam kuna uhaba wa nyumba laki nne. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pamoja na kuwepo kwa upungufu wa nyumba imeelezwa kuwa ni asilimia 15 tu ya watanzania ambao wanaweza kumiliki nyumba ambazo thamani yake ni kuanzia Sh 25 milioni 25 na kuendelea.

Hayo yameelezwa leo tarehe 9 Februar 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investiments, Dk.Fred Msemwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya taasisi hiyo.

Aidha Dk.Msemwa ameeleza kuwa bado watanzania hawajaweza kuwa na utayari wa kuwekeza katika sekta ya pesa kwa maana kuwa hawawezi kununua hisa na amana na kupelekea kuwa ni watanzania laki 8 pekee wenye kushiriki katika kuwekeza katika biashara ya fedha.

Amesema kuwa ili kuweza kuwa na nyumba bora na za bei nafuu taasisi imeona ni vyema pia watanzania wakawa na elimu ya umuhimu wa uwekezaji katika sekata ya pesa.

“Watanzania lazima wajue kuwa kuna tofauti sana ya kuwa na fedha na kuwekeza katika katika sekta ya kifedha kwani kuwekeza katika fedha na kuwa na nyumba bora na yenye gharama nafuu ni mambo ambayo yanafanana,” ameeleza Dk Msemwa.

Aidha ameeleza kuwa jumla ya nyumba zimejengwa 983 zimejengwa katika mikoa 19 ya Tanzania bara huku nyumba za gharama nafuu zikiendelea kujengwa katika mikoa yenye uhaba wa nyumba za walimu,watumishi na kada mbalimbali wenye kipato cha chini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!