Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania, China zajidili ushirikiano mifumo utoaji haki nchini
Habari Mchanganyiko

Tanzania, China zajidili ushirikiano mifumo utoaji haki nchini

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian
Spread the love

 

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro amekutana na Balozi wa China nchini Tanzania na kujadili kwa pamoja namna ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya sheria na utoaji wa haki. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Aprili tarehe 7 2022, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Waziri Ndumbaro amesema kwenye mjadala huo Serikali ya Tanzania imejifunza namna mifumo ya utoaji wa haki nchini inavyopaswa kufanya kazi.

“Tumejidili mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano wa nchi zetu kwenye sekta ya sheria na utoaji haki. ” Eneo hili ni muhimu kwa kuhakikisha uchumi amani na utulivu wa nchi vinakwenda vizuri,”…balozi ametueleza jinsi China inavyotumia mifumo ya kisheria kuhakikisha uchumi unakuwa,” amesema Ndumbaro.

Tumejaribu kuangalia kwa namna gani sheria na mfumo wa utoaji haki nchini unaweza kusaidia kukuza uchumi na biashara kati ya Tanzania ya china.

Amesema kuwa, Tanzania itajifunza mengi kutoka kwa wataalamu wa masuala ya sheria kutoka nchini China watakaokuja kutoa elimu zaidi ya utoaji haki kwa wakati wataalamu wetu pia kwenda nchini humo kujifunza zaidi.

Aidha amesema ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pia ni muhimu… tunatakiwa kuwa na ofisi ya DPP katika kila Wilaya, lakini mpaka sasa Tanzania ina upungufu wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwenye Wilaya 125.

“Tunatakiwa kuwa na Ofisi za DPP kila Wilaya, sasa tuna upungufu wa ofisi 125 ambazo tunapaswa kujenga lakini tumeongea na balozi hapa na tumeanza majadiliano namna China inavyoweza kutusaidia kwenye ujenzi huo sambamba na kutoa mafunzo kwa wataalamu watakaokwenda kufanya kazi kwenye ofisi hizo”

Amesema kuwa hatua hiyo itaondoa msongamano wa kesi pamoja na mahabusu.
“Tunaamini Ofisi hizo zikiwepo tutaongeza kasi ya utoaji haki na kupunguza msongamano wa kesi na malalamiko”

Amesema kuwa Balozi wa China amepokea maombi hayo na kwamba wataalamu kutoka nchi zote mbili watakutana kujadili kwa undani.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema kuwa nchi hizo mbili zimejadili mambo muhimu ya kuhakikisha mifumo ya utoaji haki inaimarika.

“Leo nimefurahi kukutana na Waziri wa Katiba na Sheria tumejidili na tumebadilisha uzoefu wa nchi zetu juu ya mahusiano kisheria na kikatiba”

Amesema kuwa nchi hizo zimekuwa zinaurafiki wa muda mrefu, na kwamba furaha ya China ni kuona Tanzania yenye mifumo mizuri Hususan ya kisheria.

1 Comment

  • China haina haki. Sasa tunawapa sheria zetu watufundishe kunyanyasa watanzania wenzetu au?
    Pia, kwanini hatutumii nchi zigine zilizobobea vyama vingi. Hawa hawana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!