Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tanroads Arusha yaendesha bomoabomoa kupisha upanuzi wa barabara kuu
Habari Mchanganyiko

Tanroads Arusha yaendesha bomoabomoa kupisha upanuzi wa barabara kuu

Barabara ya kiwango cha rami
Spread the love

 

WAKALA wa Barabara nchini – Tanroads mkoa wa Arusha imeanza kutekeleza zoezi la kubomoa vibanda vilivyojengwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuu ya Arusha hadi Makuyuni ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo. Anaripoti Joseph Ngilisho, Arusha … (endelea).

Akizungumza na wananchi katika eneo la Kisongo wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo lililoibua taharuki kwa wafanyabiashara wadogo, Meneja wa Tanroads mkoa wa Arusha, Regnald Masawe alisema wananchi waliovamia na kujenga vibanda ndani ya hifadhi ya barabara hawana uhalali na eneo hilo na wanapaswa kuondoka mara moja.

“Leo tupo hapa kwa ajili ya kuondoa vibanda wananchi wanapaswa kuelewa kwamba yoyote aliyejenga kibanda ndani ya eneo la mita 30 kutoka katikati ya barabara ametenda kosa na anapaswa kuchukuliwa hatua na leo tumeanza kuviondoa vibanda hivyo,”

Aidha, alisema kwamba eneo la hifadhi ya barabara ni moja ya maeneo hatarishi kwa yoyote atakayekimbilia kulitumia kwa kuwa hatakuwa na uhakika wa maisha yake na mali zake hasa kunapotokea gari kuacha njia.

Alisema mpango wa serikali katika maeneo hayo ya hifadhi ya barabara ni pamoja na kujenga vituo vya magari nje ya barabara kuu ili kuepusha magari makubwa kuegeshwa barabarani na kusababisha msongamano.

“Sisi kama wakala wa barabara tumepanga kujenga standi nje ya barabara kuu katika maeneo yenye uhitaji ili kurahisisha magari kushusha abiria na kupakia bila kubughudhi watumiaji wengine wa barabara,” alisema.

Masawe alisisitiza kwamba yeyote anayefanya biashara kwenye barabara ya akiba ni kinyume cha sheria kwa kuwa watu wanatakiwa kukaa umbali wa mita 30 kutoka katikati ya barabara.

Mbali na ujenzi wa stendi ya magari, maeneo hayo ya hifadhi ya barabara, Tanroads imepanga kuanza kuotesha miti na kutengeneza barabara za Watembea kwa miguu.

Baadhi ya wananchi katika eneo hilo la Kisongo ambao waliathiriwa na bomoabomoa hiyo waliipongeza Tanroads kwa kuboresha miundo mbinu yake ila waliomba wasiharibiwe mali zao na kuomba waongezewe muda wa kufanya biashara ndogondogo bila kuweka vibanda.

“Kwa kweli hivi vibanda havistahili kuwepo kando ya barabara kuu na mimi naunga mkono zoezi hilo ila naomba hawa wafanyabiashara hususani kina mama wanaouza mbogamboga na matunda waachwe waendelee kuuza bila kuweka vibanda,” alisema Charles Lobulu mkazi wa Kisongo.

Hata hivyo, Meneja huyo wa Tanroads, alikubali ombi hilo na kutoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara hao wa mbogamboga na matunda kuendelea kuuza bidhaa zao hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!