August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanga waanza kutumbuana

Spread the love

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, Tanga limewasimaisha kazi watumishi wawili  na wengine wawili kupewa adhabu kwa madai ya ukikwaji wa taratibu za utumishi wa umma, anaandika Christina Haule.

Akiwasilisha uamuzi uliofikiwa na Baraza la Madiwani, Idrisa Omary Mgaza, Mwenyekiti wa Ujenzi, Uchumi na Mazingira amesema kuwa, kwa kuzingatia kanuni za utumishi na kwa mujibu wa kifungu cha 42 sheria ya mwaka 2003, adhabu hizo moja wapo inaweza kutumika ikiwemo kufukuzwa kazi, kushushwa cheo au kukatwa mshahara.

Mwenyekiti huyo amesema watumishi hao wanakabiliwa na tuhuma ya utoro kazini pamoja na kushindwa kusimamia shughuli za miradi ya maendeleo iliyomo kwenye halmashauri kwa kipindi kirefu.

Mgaza amesema kuwa, watumishi waliofukuzwa kazi ni Deogratius Gabriel kutoka Idara ya Afya, Abdallah Mkandhe ambaye alikuwa Ofisa Kilimo Msaidizi.

Amesema, watumishi hao bila ruhusu yoyote ya mwajiri, hawakuonekana kazini na kuwa wote kwa pamoja walishindwa kutoa utetezi kwa tuhumu iliyowakabili.

Baraza hilo pia limemchukulia hatua za kinidhamu Habibu Kilobwa, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamaleni Kata ya Pagwi kwa tuhuma za kutosimamia ipasavyo shughuli za maendeleo ikiwemo kutoitisha mikutano ya hadhara na kutosoma taarifa za mapato na matumizi.

Mtumishi wa nne ni Casbeth Kaale, aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Negelo ambaye alikutwa na tuhuma ya utoro kwa kipindi kirefu na kufanya shughuli za maendeleo kusimama kwa kukosa usimamizi wake.

Seleman Liwowa, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kuchukua hatua hiyo na kuongeza kuwa, uamuzi huo ni muhimu hasa kwa wale wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

error: Content is protected !!