August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Tanga sasa shwari’

Spread the love

WAKAZI wa Tanga wametakiwa kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa maelezo kuwa, ‘Tanga sasa ipo shwari, anaandika Regina Mkonde.

Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Tanga ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa ushirikiano wa asasi za kiraia wenye lengo la kusimamia utawala bora na maendeleo.

Mkutano huo uliandaliwa na mtandao wa asasi za kiraia katika Mkoa wa Tanga ambapo Shigela amesema, tishio la kuwepo kwa vitendo vya kihalifu vimetokomezwa kwa zaidi ya asilimia 80.

Kwenye hotuba yake iliyosomwa na Thobias Mwilapwa, Mkuu wa Wilaya ya Tanga ameeleza kuwa, operesheni kali imekuwa ikiendelea katika Mapango ya Amboni na kutokomeza kabisa viashiria vya vitendo hivyo.

Amesema kuwa, operesheni hiyo inaendelea katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na katika Kitongoji cha Mabatini.

Hata hivyo, kwenye hotuba hiyo Shigela ameagiza asasi hizo ziwajengee uwezo wananchi kwa lengo lwa kuwa na nafasi ya kutambua majukumu yao katika kulinda usalama wa mkoa huo ili maendeleo.

 

error: Content is protected !!