May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanesco yaomba radhi, yaeleza huduma za luku zinapopatikana

Spread the love

 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limewaomba radhi wateja wake kutokana na ukosefu wa huduma ya ununuzi wa luku kwa njia ya mtandao na kusema, huduma hiyo, inapatikana ofisi zake za mikoa na wilaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Huduma hiyo, imekuwa adimu kwa siku ya tatu na leo Jumatano, tarehe 19 Mei 2021, Tanesco imetoa taarifa ikisema, huduma hiyo kwa sasa inatikana ofisi za mikoa na wilaya.

Limesema, wataalamu wa shirika hilo, wanaendelea na kazi ya utatuzi wa manunuzi kupitia njia za kielektroniki.

“Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wakiendelea na kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa,” imeeleza taarifa hiyo ya Tanesco huku ikiongeza “tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.”

error: Content is protected !!