October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TANESCO yaghairi matengenezo mfumo wa LUKU

Spread the love

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeahirisha zoezi la matengenezo kinga ya mfumo wa ununuzi wa umeme LUKU ambalo lingesababisha kusitishwa kwa huduma hiyo kuanzia tarehe 22 hadi 25 Agosti, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Uamuzi huo umekuja leo tarehe 17 Agosti, 2022, saa chache baada ya kutoa taarifa kwa umma kuwa huduma ya LUKU haitapatikana kwa siku nne kupisha matengenezo hayo, hali iliyoibua taharuki kwa watumiaji wa nishati ya umeme nchini.

“Shirika la umeme Tanzania linawatangazia watanzania wote kuhusu kuahirisha zoezi la matengenezo kinga ya mfumo wa LUKU kama ilivyotangaza mapema leo. Tutawajulisha pale itakapokuwa tayari kuendelea na zoezi hilo,” imeeleza taarifa ya TANESCO iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilinao na Masuala ya Umma Makao Makuu.

error: Content is protected !!