March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tanesco wamdharau Naibu Waziri Kalemani

Mitambo ya kufua umeme ya Tanesco. Picha ndogo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medadi Kalemani

Spread the love

SIKU moja baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medadi Kalemani kupiga marufuku umeme kukatika katika jiji la Dar es Salaam, leo umekatika tangu asubuhi katika maeneo, mbalimbali ya jijini, anaandika Mwandishi Wetu.

Pamoja na kuwepo kwa agizo hilo la Naibu Waziri, Kalemani, lakini umeme umekatika baadhi ya maeneo ya jiji kama Kinondoni, Mwananyamala, Kigamboni na Mikocheni.

Kalemani jana alikaririwa akisema kuwa Tanesco ina vifaa vya kisasa na kwamba hatarajii kuona kunakuwepo na matatizo yaliyozoeleka ya kukatika umeme.

Miongoni mwa maagizo yaliyopuuzwa na watendaji wa chini ni lile lililotolewa na Rais John Magufuli la kutaka Dawasco kimaliza tatizo la maji jijini Dar es Salaam pamoja na lile la kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

error: Content is protected !!