December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanesco Mwanza lapongeza wafanyabiashara

Spread the love

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), Kanda ya Ziwa limeeleza kuwa, wafanyabiashara wakubwa ni miongoni mwa watu wanaongoza kulipa bili ya umeme kwa asilimia 50. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 12 Juni 2019 na Meneja wa Tanesco kanda hiyo, Mhandisi Maclean Mbonile na kwamba, Tanesco kanda hiyo imekuwa ikikusanya kiasi cha Sh. 10 Bilioni kwa mwezi ambapo wafanyabiashara wakubwa hutoa Sh. 5 Bilioni.

Amesema, kiasi cha asilimia 50 kilichobaki ndicho kinachotolewa na wananchi wa kawaida na kuwa, bado wafanyabiashara hao ni nguzo muhimu kwa shirika hilo.

“Tuna jumla ya wateja 318, 824 katika wateja hawa, wateja wetu wakubwa ni 326 na hawa waliopo kwenye kikao leo ni wateja 50 ambao wanachangia mapato ya shirika kwa kanda ya ziwa kwa asilimia 50.

“Wateja wengine 318, 498 wanachangia asilimia 50 iliyobaki, hivyo wateja hawa ni muhimu kwetu kwani wanatupa mapato makubwa na tunatambua umuhimu wao,” amesema Mhandisi Mbonile.

Amesema, mpango wa Tanesco ni kuona wafanyabiashara na wananchi wote wanapata umeme wa uhakika, ili kuendelea kufanya uzalishaji kwa uhakika.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Christopher Kadio amesema, kutokana na Tanesco kuwa na umuhimu mkubwa katika kuchangia ukuaji wa pato la Taifa, wamejipanga kuondoa hujuma zilizopo ikiwemo ya uhalibifu wa miundombinu.

“Hizo wilaya zilikuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, tayari hujuma hizo tumezifanyia kazi na sasa hali ipo vizuri,” amesema Kadio.

error: Content is protected !!