Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Biashara TANESCO kuvuna bilioni 5 mapato ya mwezi kutoka GGML
BiasharaHabari Mchanganyiko

TANESCO kuvuna bilioni 5 mapato ya mwezi kutoka GGML

Spread the love

KUKAMILIKA kwa mradi wa kupeleka umeme kwenye Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kunatarajiwa kutaliwezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupata kiasi cha Shilingi bilioni tano kwa mwezi zitakazotokana na mauzo ya umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamebanika juzi tarehe 21 Februari, 2022 wakati wa shughuli ya utiaji saini mkataba wa mauziano ya nishati ya umeme baina ya TANESCO na GGML.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika mjini Geita, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Maharage Chande amesema kuanza kwa biashara hiyo kutaiwezesha TANESCO kuongeza mapato yatakayosaidia kuboresha huduma mbalimbali kwa wateja wao.

“Maana ya pili tutapunguza uzalishaji wa hewa chakafu ya dizeli, lakini pia kuongeza ufanisi wa kazi zao GGML kwa maana ya gharama za uzalishaji zitapungua” alisema Maharage.

Aliongeza kuwa, hatua hiyo kubwa na muhimu ya GGML kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa imefikiwa baada ya miaka zaidi ya ishirini tangu kuanzishwa kwa kampuni ya GGML.

Kufanikiwa kwa jambo hilo kumetokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na TANESCO katika kuimarisha upatikanaji wa umeme ndani ya Mkoa wa Geita kwa kujenga kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mpomvu chenye uwezo wa megawati 90.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa GGML, Simon Shayo amesema GGML watajenga kituo cha kupokea na kupoza umeme ambazo zitatumika kwa matumizi ya mgodi.

“Kwetu sisi tunapunguza gharama za uzalishaji wa umeme tunao utumia kwa maana kwa kuacha kutumia mafuta lakini pia kutunza mazingira, Dunia sasa inatoka kwenye matumizi ya mafuta ambayo yanazalisha hewa ya ukaa” amesema Shayo.

Kampuni ya GGML kwa sasa inatumia Dola za kimarekani senti 19 kuzalisha umeme kwa unit moja kwa kutumia mafuta, lakini mradi huo ukikamilika na kuunganishwa na gridi watatumia senti 9 za kimarekani kwa unit moja kupata umeme.

Mradi huo wa kupeleka umeme GGML unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu, ambapo utajumuisha njia ya kusafirisha umeme umbali wa kilometa 6 na kituo cha kupoza umeme cha GGML cha kilovolt 33.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!