Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Tanesco hoi kwa madeni
Habari Mchanganyiko

Tanesco hoi kwa madeni

Makao Mkuu wa Tanesco, Ubungo Dar es Salaam kabla hayajavunjwa
Spread the love

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme la taifa (Tanesco), linakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni kutoka kwa makampuni ya kufua umeme. Hadi Januari mwaka jana, deni la Tanesco lilikuwa limefikia kiasi cha Sh. 630.8 bilioni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Miongoni mwa makampuni yanayoidai Tanesco mabilioni hayo ya shilingi, ni pamoja na Pan African Energy Tanzania Limited (Songas), kampuni ya kufua umeme kwa njia ya gesi ya Songas na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula, ameliambia Bunge mjini Dodoma, kwamba deni dhidi ya Tanesco limeathiri sana utendaji kazi wa TPDC.

Amesema, hatua ya Tanesco ya kutolipa kulipa deni lake kwa TPDC kwa wakati, imesababishia shirika hilo, kushindwa kuwekeza kwenye miradi mingine.

Kitandula alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya kamati yake bungeni jana Jumatano.

Alisema, “serikali iangalie namna ya kufanya majadiliano na makampuni yaliyoingia mikataba na shirika hilo, kwa kutumia sheria za sasa za rasilimali. Hii itasaidia kuboresha kasi hasa katika mikataba ya gesi kati ya Tanesco, TPDC, Songas na Pan African Energy.”

Alisema, “deni linalofikia Sh. bilioni 630.8, zilizokuwa zikidaiwa na Songas, PAET na TPDC, zinaweza kuziangamiza kabisa makampuni yanayofanya biashara na Tanesco n ahata Tanesco lenyewe.”

Naye mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy, akichangia mjadala huo alisema, mkataba kati ya Tanesco na Song’as, hauna manufaa kwa taifa na hivyo, akamtaka Rais John Magufuli, kuuvunja mara moja. Kessy aliita mkataba huo kuwa kinyonyaji.

Alisema, mpaka sasa, serikali tayari imekwapuliwa takribani Sh. 1.3 trilioni na kampuni hiyo, wakati mtaji na dhamana vya mkopo wa ujenzi wa mradi wa Song’as vimetolewa na serikali.

Serikali kupitia Tanesco, ilijifunga katika mkataba wa kinyonyaji wa kufua umeme na kampuni wa Song’as na Independent Power Tanzania Limited (IPTL), mwaka 1994. Mikataba hii, ilijadiliwa kwenye baraza la mawaziri na kufikia makubaliano yaliyoazaa mikataba ambayo ni katili na matokeo yake ni mzigo usiobebeka wa gharama ya umeme.

Taarifa zinasema, Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), viliona uchungu na kushauri serikali ivunje mikataba hiyo.

Msingi wa ushauri huo ni kwamba mkataba ulifungwa kutokana na shinikizo la rushwa zilizotolewa kwa baadhi ya watendaji serikalini.

Mkataba huu, hata katika mazingira ya soko huria, unaipa kampuni hiyo hodhi ya shughuli za upakuaji na upakiaji na mkataba wake uliongezewa kinyemela, miaka10 hata kabla kipindi chake cha kwanza hakijamalizika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Makamba: China ni ya mfani kwa kupunguza umaskini

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, January...

error: Content is protected !!