Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu TAMWA yalaani tuhuma za ngono UDOM yaipa ujumbe Takukuru
ElimuHabari Mchanganyiko

TAMWA yalaani tuhuma za ngono UDOM yaipa ujumbe Takukuru

Spread the love

 

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA) kinalaani tukio la Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Peter Mswahili kutuhumiwa kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa kike chuoni hapo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Jana Alhamisi, tarehe 28 Oktoba 2021, uongozi wa UDOM ulitoa taarifa ya kusimamishwa kwa mhadhiri huyo ili kupisha uichunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Ni baada ya taarifa zake, kusambaa mitandaoni zikimwonesha akiwa na mmoja wa mwanafunzi chumbani. Mhadhiri huyo anatuhumiwa kuwafelisha wanafunzi na ili ufaulu, inaelezwa anahitaji rushwa ya ngono.

Leo Ijumaa, tarehe 29 Oktoba 2021, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA,
Dk Rose Reuben amesema, chama hicho kinapinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake ikiwamo rushwa ya ngono, “tunalaani tukio hilo linalovunja maadili ya utumishi wa umma na zaidi hasa kudhalilisha watoto wa kike katika taasisi hii ya elimu ya juu..”

“Kadhalika, TAMWA tunasikitishwa na vitendo hivyo ambavyo sio tu vimekuwa chanzo cha kuharibu mustakabali wa kitaaluma wa watoto wa kike, lakini pia ndicho chanzo cha magonjwa ya kuambukiza, sonona na kurudisha nyuma kundi hilo,” amesema.

Chuo Kikuu cha Dodoma

Amesema, Mwaka 2019 TAMWA ilifanya tathmini ya kuangazia ukubwa wa rushwa ya ngono kwenye vyumba vya habari, maeneo ya kazini na taasisi za elimu ya juu, na kubaini kuwa tatizo hilo lipo kwa ukubwa wake.

Aidha, TAMWA ilibaini ukimya umetawala kwa wale waathirika wa rushwa ya ngono kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo woga wa kukosa vibarua, kufukuzwa shule au kufeli mitihani yao.

“Hivyo tunalaani vikali vitendo hivi huku tukiupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuchukua hatua za haraka dhidi ya mhadhiri huyo lakini pia tunaushauri uongozi wa chuo hicho kuweka mikakati itakayokomesha vitendo hivyo,” amesema

Dk. Reuben amesema, TAMWA inaomba pindi uchunguzi utakapokamilika basi sheria ichukue mkondo wake ili iwe funzo kwa wahadhiri wengine wanaoharibu watoto wa kike.

“Pia, tunaiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iendelee kushirikiana na wadau kutoa elimu kuhusu rushwa ya ngono na udhalilishaji mwingine wa kijinsia.‘Digrii bila rushwa ya ngono, ni digrii yenye tija,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!