October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tamwa yaiomba serikali kutunga sera ya familia

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Rose Reuben

Spread the love

 

CHAMA Cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (Tamwa), kimeishauri serikali kuanzisha sera maalum ya familia ili kukabiliana na changamoto zinazoibuka kwenye jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi wa Tamwa Rose Reuben alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Rose amesema kuwa Sera hiyo itakuwa suluhisho la matatizo mengi kwenye jamii kwa kuwa itasaidia kuungoza wanafamilia.

Familia ni ngazi muhimu kwenye jamii kila ambacho kipo jamii chanzo chake unatokana na familia.

Amesema kuwa jukumu la Tamwa ni kutetea wanawake , na watoto kwenye jamii hivyo ni muhimu serikali kuwepo kwa sera itakayowezesha utetezi kwa msingi wa awali wa watu kujua wajibu kupita sera.

Wakati huo huo amesema kuwa Tamwa imejikita kwenye utetezi wa haki jinsia “Shirika letu linafanya kazi ya kuwatetea wanawake, wasichana na watoto kupita vyombo vya habari, tumekuwa mstari wa mbele kumtetea watoto wa kike kurejeshwa shuleni wanapopata mimba tukieleza jamii kuwa kuna sabab nyingi zinazopelekea mtoto wa kike kupata mimba akiwa shule.

Licha ya kukiri kuwa zipo sababu za uzembe zinazopelekea watoto kupata mimba amesema kuwa kuna sababu nyingi zinazopelekea watoto wa kike kupata mimba wakiwa shule pamoja na sababu za hali duni za kimaisha, au kufanyiwa ukatili wa kubakwa.

Amesemesema kuwa Taasisi hiyo imepaza sauti juu ya suala la ndoa za utotoni “kutokana na mila na desturi potofu baadhi ya familia zinaozesha mabinti zao wakiwa watoto na kwamba kitendo hicho kinapelekea watoto hao kunyimwa haki yake ya kupata elimu”.

Amesema kuwa utetezi wa mtoto wa kike unamaana ya kumfanya mwanamke kunufaika kwa kukaa kwenye nyazifa itakayopelekea kuwa mtoa uamuzi kwenye ngazi mbalimbali nchini.

Amesema kuwa Tamwa ina mpango mkakati wa miaka mitano ulioanza mwaka jana wenye nia ya kuifanya Tanzania inakuwa salama isiyokuwa na ukatili wa kijinsia, makundi yanayoachwa nyuma kiuchumi, isiyokuwa na watu ambao wanajihisi hawapo salama kwa mfano wazee wenye macho mekundu wakadhulumiwa maisha yao kwa madai wao ni wachawi , watu wenye ulemavu wa albino ambapo wakuwa wakifanyiwa dhuluma ya kukatwa viongo vyao kwa Imani za kishirikina.

Ametoa wito kwa serikali kwa kubadilisha sharia itakayoeleta unafuu kwa wanawake na watoto kwa mfano sera ya familia , ‘’hapa tanzania hatuna sera ya familia hii sera ya familia ni muhimu , sera hii itapunguza matatizo mengi nje na ndani ya family itasaidia jamii na kwamba wanafamilia watajua wajibu wao.

error: Content is protected !!