February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TAMWA: Pombe chanzo cha ukatili

Spread the love

CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kupitia Kituo cha Usuluhishi (CRC) kimeitaka serikali kurekebisha baadhi ya vifungu vya sheria ya vileo, kuandaa sera ya kitaifa ya masuala ya matumizi ya pombe ili kudhibiti matendo ya kikatili, anaandika Regina Mkonde.

Kwa mujibu wa chama hicho, pombe matendo ya kikatili kwenye jamii husababishwa na unywaji pombe kupita kiasi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Loyce Gondwe, Mwanasheria wa TAMWA, , amesema kukinzana kwa baadhi ya vifungu vya sheria ya vileo pamoja na kutofuatiliwa kwa sheria hiyo, kumesababisha ongezeko la utumiaji pombe kupita kiasi kwenye jamii.

“Hakuna sera ya kitaifa inayodhibiti unywaji pombe kupita kiasi, sheria zilizopo zinazungumzia zaidi uzalishaji na leseni na si kudhibiti matumizi ya pombe kupita kiasi,” amesema Gondwe.

Ameongeza kuwa, vitendo vya rushwa vimevyokithiri kwa baadhi ya watu wenye mamlaka ya kudhibiti ama kuangalia muda uliopangwa kisheria wa kuanza na kumaliza kuuzwa kwa pombe.

Kwa upande mwingine Gladness Munuo, Mratibu wa kituo hicho (CRC) amesema unywaji pombe kupita kiasi umepelekea ongezeko la matendo ya kikatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ikiwemo ubakaji, vipigo kwa wanawake na mimba katika umri mdogo.

“Unywaji pombe kupita kiasi umesababisha ongezeko la ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto, ikiwemo kutelekezwa kwa wanawake na watoto na migogoro ya ndoa na familia,” amesema Munuo.

Munuo ameongeza kuwa, ni wakati wa serikali kuandaa mikakati na sera ya kudhibiti matumizi ya pombe kupita kiasi ili kuijenga Tanzania yenye amani inayochukia ukatili wa kijinsia.

Kituo cha CRC kinadhaminiwa na shirika lisilo la kiserikali la IOGT la nchini Sweden, lengo la kituo hiki ni kuhakikisha kuwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji pombe kupita kiasi wanapata msaada na hali hii inatokomoea nchini.

CRC kinashirikiana na jamii, dawati la kijinsia, afisa ustawi wa jamii, viongozi wa kata pamoja na waandishi wa habari kuripoti wahanga na kuwachukulia hatua wahalifu watakaobainika.

Hata hivyo Mohamed Chunga, mwanaharakati wa haki za jamii, ameitaka serikali kuweka mazingira magumu ya upatikanaji wa pombe ili kunusuru watoto waliochini ya umri wasinywe pombe

“Serikali haiko makini katika ufuatiliaji wa sheria, ndiyo maana unaona ongezeko la baa katika maeneo yasiyo ruhusiwa kisheria.

Chunga amewataka wananchi kukemea ujenzi wa baa katika maeneo ya makazi ya watu hasa shule na hospitali sababu itasaidia kuleta vishawishi kwa wanywaji wa pombe watakapotumia umbali mrefu kutafuta pombe.

error: Content is protected !!