Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tamisemi yamkalia kooni Boniface Jacob
Habari za Siasa

Tamisemi yamkalia kooni Boniface Jacob

Spread the love

NAIBU Waziri wa  Ofisi ya Rais, Tawala za  Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) nchini Tanzania, Mwita Waitara amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kufanya uchunguzi wa upotevu wa Sh.1.6 bilioni, zilizoibuliwa na Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa Halmashauri ya Ubungo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endeelea).

Wiki iliyopita, Jacob akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam alisema, miongoni mwa sababu zilizotumika kumwondoa madarakani ni jitihada zake za kuibua ufisadi bilioni hizo za fedha.

Jacob amepoteza nafasi ya umeya baada ya barua inayoelezwa kuandikwa tarehe 28 Aprili 2020 na katibu wa Chadema Kata ya Ubungo kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri kuonyesha amevuliwa uanachama hivyo kupoteza sifa za kuwa meya.

Hata hivyo, Jacob mwenyewe, Chadema makao makuu na mtu huyo ambaye jina lake lilitumika kwenye barua hiyo kudai haina ukweli kwani hakuna kikao chochote kilichokaa cha kumjadili Jacob kisha kumvua uanachama.

Akizungumza na MwanaHALISI Online  leo Jumatatu tarehe 11 Mei 2020, Waitara amesema kama kumetokea wizi au upotevu wowote wa fedha kwenye Halmashauri hiyo ni lazima Meya ahusike kwa kuwa yeye ni sehemu ya watia saini.

Amesema hakuna malalamiko yoyote yaliyofikishwa ofisi ya mkuu wa mkoa au katibu tawala wa mkoa kuhusu upotevu wa fedha hizo.

Waitara amesema kwa kuwa Jacob ametoa tuhuma hizo hadharani, atakuwa na vithibitisho hivyo ameagiza uchunguzi ufanyike na watakaobainika hatua zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika ikiwamo Jacob mwenyewe.

“Serikali inafanya uchunguzi zaidi na kwamba itamchukulia hatua  kwa upotoshajikwa sababu yeye kipindi chote tangu mwaka 2016 alipokuwa Meya asisema kama kuna upotevu mpaka pale chama chake kilipomvua uanachama ndio aseme,” amesema Waitara

“Jacob ni kama mfamaji tu, haishi kutapata…yeye ni sehemu ya watia saini wa miradi yote ndani ya Halmashauri, hivyo ni lazima itakuwa kahusika kwenye upotevu huo,” amesema Waitara.

Baada ya Jacob kung’olewa katika nafasi hiyo, Tamisemi ilimweleza ana njia mbili za kuchukua ambazo ni kufungua kesi mahakamani au kukata rufaa kwa waziri wa Tamisemi.

Waitara akijibu swali la MwanaHALISI Online lililotaka kujua kama barua imekwisha kufika amesema hadi leo Jumatatu asubuhi ilikuwa haijafika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!