July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tamisemi yaboresha ukusanyaji wa kodi

Spread the love

OFISI ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI, imeboresha huduma ya makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali za mamlaka za serikali za mitaa kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa Local Government Revenue Colletion Information System (LGRCIS). Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza leo na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, kuhusu mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato ya mamlaka za Serikali za Mitaa, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini ofisi ya Waziri Mkuu, OWM-TAMISEMI, Rabeca Kwandu amesema mfumo huo ni moja ya maboresho ya kusaidia kuongeza mapato ya mamlaka zake.

Kwandu ameeleza malengo makuu ya kuanzisha mfumo huo wa “Local Government Revenue Colletion Information System (LGRCIS), kuwa ni pamoja na kupata taarifa za walipa kodi wa mamlaka za Serikali za Mitaa na kuhifadhi kwa usahihi katika kanzi data ya mfumo pamoja na kupata takwimu sahihi ya vyanzo vya mapato.

Amesema kuwa utafiti uliofanyika na Ofisi hiyo uligundua hakukuwa na mfumo wa kielektroniki wa kurahisisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya halmashauri hivyo kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya kodi ukilinganisha na makisio yaliyopangwa

Amesema kuwa mifumo ya kielekroniki ya malipo – Electronic Payment (Mfano; Point of Sale, PoS, M-Pesa, Airtel Money, Zpes, Mabenki, MaxMalipo) ni mifumo ambayo itatumika katika mfumo wa LGRCIS itakayowezesha walipa kodi kulipa kodi na kupunguza misongamano isiyo na sababu.

“Malipo kwa njia ya miamala ya kielektroniki ni suluhisho la changamoto hizo kwani yanaongeza udhibiti, kupunguza au kuondoa mianya ya ufujaji wa mapato na kuongeza uwazi,” amesema Kwandu.

Kwa upande wa Mweka Hazina wa TEHAMA katika Jiji la Arusha, Kessy Mpakata amesema jiji hilo ni miongoni mwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na hatua kubwa waliyofanikiwa likiwa na ongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato ya jiji kutoka Tsh 5 bilioni kwa mwaka wa fedha 2012-13 hadi Sh. 10.7 bilioni kwa mwaka wa fesha 2014-15 sawa na ongezeko la 21.4.%.

Mpakata amesema kuwa mchango wa miradi ya ndani ya maendeleo umeongezeka toka Sh. 1.2 bilioni kwa mwaka 2014-13 hadi Sh. 4.8 bilioni mwaka 2014-15 sawa na ongezeko la 40.0% ambapo jumla ya Sh. 8.2 bilioni kwa mwaka 2015-16 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za mapato za ndani sawa na 63% ya bajeti yote ya mapato ya ndani.

“Ni matarajio ya OWM-TAMISEMI kuwa mfumo huu utaleta nabadiliko makubwa katika halmashauri na kuachana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali kuu,” amesema Mpakata.

error: Content is protected !!