Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Maisha Afya Tamisemi wapokea magari ya sekta ya Afya
Afya

Tamisemi wapokea magari ya sekta ya Afya

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imekabidhiwa msaada wa magari sita na shirika la USAID Global Health Supply Chain, yatakayopelekwa katika halmashauri mbalimbali nchini ili kusaidia utoaji wa huduma za afya. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari hayo Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, amesema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka ambao utasaidia kuboresha huduma za afya.

Amesema katika maeneo mengi nchini kumekuwepo na changamoto ya huduma za afya kutokana na jiografia ya maeneo husika.

Jafo amesema kuwa kupatikana kwa magari hayo sita kutasaidia halmashauri zile ambazo zipo katika mazingira magumu kijiografia ili kuwawezesha wataalamu wa afya kuvitembelea vituo mbalimbali vinavyotoa tiba.

“Magari haya yatatumika pia katika kukuza kiwango cha utoaji wa chanjo katika maeneo mbalimbali ambayo bado yapo chini kutoka na jiografia ya maeneo hayo, kuna baadhi ya maeneo nilisha wahi kupita nikakuta hayajawahi kutembelewa na mtaalamu wa afya kwa miaka tisa, kuna eneo kama Nanyumbu Dmo anakwenda kufuata vifaa kwa baiskeli,” amesema Jafo.

Hata hivyo amesema magari hayo yatumike kwa matumizi ya masula ya afya na siyo vinginevyo kwani hatua kali zitachukuliwa kwa ataye husika.

“Leo hii haya magari tunayoyakabidhi sitaki kusikia kuwa yanakwenda kwajili ya matumizi mengine tofauti na masuala ya afya,yasitumike kwa shughuri nyingine kama vile ukusanyaji wa kodi pamoja na kutumika kama usafiri wa mwenyekiti wa halmashauri,” amesema Jafo.

Aidha amesema kuwa katika kuboresha sekta ya afya nchini tayari vituo 210 vyenye uwezo wa kufanya upasujai vimeshajengwa na serikali katika halmashauri mbalimbali nchini.

Amesema toka Tanzania ipate uhuru mwaka 1961 hadi mwaka jana jumla ya vituo 115 ndivyo vilikuwa vianaweza kutoa huduma za upasuaji lakini hivi sasa wamevunja rekodi hiyo kwa miaka miwili iliyopita kwa kujenga vituo 210 vyenye uwezo wa kutoa huduma hiyo.

Aidha amesema pia serikali tayari imeshatenga Sh. Bilioni 38.9 kwajili ya ujenzi wa vituo vingine vipya 98 ambavyo vitasaidia katika kuboresha huduma ya afya nchini.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID Global Health Supply Chain, Mavere Tukai, akikabidhi magari hayo amesema kuwa msaada huo wa uliotolewa ni katika kuwezesha suala la utoaji huduma za afya nchini.

Amesema lengo lao ni kuhakikisha kuwa wanashirikia na serikali katika kuwezesha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya kwa jamii katika mazingira rafiki.

Magari hayo sita yatapekwa katika halmashauri ya wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara,Chemba mkoani Dodoma, Tanganyika mkoani Katavi, Kigoma, Longido Arusha na ofisi ya Rais Tamisemi.

Hata hivyo alipiga marufuku kwa wakuu wa idara ya afya kutumia magari hayo kinyume na malengo, alisema itakuwa ni jambo la ajabu kutumia magari hayo kukusanyia mapato(Uchuru), kuwabebea madiwani au mwenyekiti wa halmashauri husika.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the loveMADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi...

Afya

Kipindupindu chabisha hodi Dar, wagonjwa 10 waripotiwa

Spread the love  Ugonjwa wa Kipindupindu umeibuka jijini Dar es salaam ambapo...

Afya

Ujenzi wa zahanati kwa ufadhili wa TASAF wafikia asilimia 95

Spread the love  UJENZI wa mradi wa Zahanati ya Mwanalugali A Kibaha...

Afya

Serikali yatenga Sh. 15 bilioni kukamilisha maboma 300 ya zahanati

Spread the love  SERIKALI imetenga kiasi cha fedha Sh. 15 bilioni, katika...

error: Content is protected !!