WIZARA Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imezindua mfumo wa kidigitali wa usimamizi asilimia 10 ya fedha za mapato ya halmashauri zinazotolewa kwa wananchi kwa ajili ya mikopo ya vikundi maalumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, leo Jumanne, tarehe 24 Mei 2022, jijini Dodoma, Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amesema mfumo huo utasaidia kudhibiti vitendo vya ubadhirifu wa fedha hizo.
“Maelekezo ya CAG kwenye yale maeneo ambayo tumeelekezwa TAMISEMI ni suala la asilimia 10 ya fedha za vikundi na usimamizi kwani limekuwa jambo ambalo linajirudia kwenye hoja zake, lakini pia Bunge kupitia kamati ukiangalia maoni na mapendekezo kila mwaka yamekuwa hay ohayo,” amesema Bashungwa.
Bashungwa amesema “kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, tumeona hii ndiyo njia sahihi ya kutatua kero hii, si jambo dogo kuunda mfumo ambao unatumia dijitali katika kusimamia hizi fedha na ndivyo tunavyotakiwa kufanya. Mifumo hii ambayo najua imeandaliwa vizuri italeta mageuzi kwenye halmashauri zetu.”
Waziri huyo wa TAMISEMI, amesema mfumo huo umetengezwa kwa msaada wa Benki ya NMB.
Leave a comment