May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tamisemi: Hospitali Biharamulo ilitengewa Mil 500

Hospitali ya wilaya ya Biharamulo

Spread the love

 

HALIMASHAURI ya Wilaya ya Biharamulo, Kagera ilipatiwa kiasi cha Sh. 500 Milioni katika mwaka wa fedha 2019\20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya hiyo. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).  

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 20 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Maelezo hayo yametolewa baada ya Ezra Chilewesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, kuiomba serikali ieleze, kiasi cha Sh. 1 Bilioni kitatolewa lini ili kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo.

“Serikali ilitoa Sh. 500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo, lakini kiasi cha Sh. 204 Milioni kilirejeshwa baada ya kufunga mwaka wa fedha – Julai 2020,” imeeleza Tamisemi.

Tamisemi imeeleza, jengo la wagonjwa wa nje, maabara na majengo yote mawili, yamefikia asilimia 80.

“Kati ya fedha hizo zilitolewa, Sh. 204 milioni zilirejeshwa kwenye mfuko mkuu wa serikali baada ya kuvuka mwaka wa fedha 2019/20, tarehe Juni 30, 2020 kwa mujibu wa sheria ya bajeti ya fedha ya mwaka 2015 na kanuni zake mwaka 2015.

“Mwezi Januari 2021 serikali imetoa Sh. 1 Bilioni kwa Halmashauri ya Biharamulo ili kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri. Majengo yatakayojengwa ni jengo la utawala na jengo la wazazi ambayo yamefika asilimia 40 ya ukamilishaji.

“Pia jengo la kuhifadhi dawa na jengo la kufulia ambayo yamefika asilimia 60 ya ukamilishaji. Katika mwaka wa fedha 2021/22 hospitali hiyo, imetengewa Sh. 300 milioni,” amesema.

error: Content is protected !!