June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tamaa ya cheo imempeleka Mtolea CCM

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Abdual Kambaya (wa pili kulia)

Spread the love

HAMAHAMA ya wabunge, madiwani na wanasiasa wa upinzani ndani ya vyama vyao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) imeelezwa kuwa inasababishwa uroho wa nyadhifa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Abdallah Kambaya amesema kuwa wabunge na madiwani wamekimbia vyama vya upinzani na kujiunga na chama tawala ili watafute fursa za watawala.

Kuhama kwa Mbunge wa Temeke ambaye alijinasibu kuwa yeye sio manafki na hatohama upinzani.

Amesema kuwa Mtolea hana sababu za msingi za Kujiunga na CCM isipokuwa ni tamaa ya nyadhfa kama ile aliyokuwa nayo Mtatiro.

Mtulia huyu huyu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kuisema serikali ya CCM kuhusu shambulio la Lissu bungeni leo ameungana na wale aliwawalalamikia.

“Mtulia alikwenda Liwale akatumia jukwaa la kampeni kumtukana Kuchauka leo hii ameenda alipoenda kuugana naye”.amesema Kambaya.

“Tabia hii ya kuhama na kusaliti imekuwa ikiendelezwa na wabunge wa CUF wanaomunga mkono Maalimu Seif Sharif Hamad ambao wamekuwa wakijinasabu kuwa wao ndio imara sisi tunatumika” amesema.

Wakati huo huo amemtaja Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF Julias Mtatiro kuwa amehama upinzani kwa tamaa ta kupata nyadhifa kama kama walivyoapa kina Katambi.

“Hii tabia ya kina Mtatiro ni Tabia ya Ujokate na Tabia ya Umakonda,” amesema Kambaya.

Kambaya amemtaja Mbunge wa Kinondoni Maulidi Mtulia kuwa alihama CUF kutokana na kutumia vibaya ubunge wake,
amedai kuwa mbunge huyu alikopa fedha nyingi alizoshindwa kuzilipa na hivyo aliamua kuhama ili anze upya na apate tena stahiki za ubunge.

error: Content is protected !!