Monday , 29 May 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Taliban wawajeruhi vibaya waandishi wa habari, DW waondoa Afghanistan
Kimataifa

Taliban wawajeruhi vibaya waandishi wa habari, DW waondoa Afghanistan

Spread the love

 

WAANDISHI wawili wa habari wawili nchini Afghanistan, wameumizwa vibaya kufuatia kushambuliwa na kundi la Taliban, baada ya kukamatwa wakipiga picha maandamano mjini Kabul, Jumatano iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Picha zilizoibuka kwenye mitandao ya kijamii, zinawaonyesha waandishi hao wakiwa na majeraha makubwa mwilini, Nematullah Naqdi na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Taqi Darybai.

Waandishi hao walikamatwa na wanamgambo wa Taliban, ambao sasa wanatawala nchi ya Afghanistan, walipokuwa wanaripoti maandamano yaliyoitishwa na wanawake, yenye lengo la kudai kuwapo usawa wa kijinsia na kushinikiza kuondoka kwa taifa la Pakistan nchini mwao.

Nematullah aliliambia shirika la habari la AFP, kwamba mmoja wa Taliban aliweka mguu wake kichwani, “akaniponda uso,’ akanipiga teke kichwani … nilidhani wataniua.”

Naqdi alikuwa akiripoti kuhusu maandamano ya wanawake mbele ya kituo cha polisi, akiwa na mwenzake Taqi kutoka gazeti la Etilaatroz.

Taliban wamepiga marufuku maandamano isipokuwa kwa idhini ya wizara ya haki.

Hata hivyo, waandamanaji kadhaa waliimba “tunataka uhuru” walipokusanyika karibu na ubalozi wa Pakistan huko Kabul na Taliban walifyatua risasi kuwatawanya, waandamanaji walisema.

Vyombo vya habari vya eneo hilo pia vimeripoti maandamano mengine ya wanawake katika mkoa wa Kapisa, kaskazini mashariki mwa Kabul.

Katika kile kinachoweza kuitwa, “kushusha pumzi,” kundi la waandishi habari wa DW nchini Afghanistan lilivuka mpaka na kuingia Pakistan hatua inayokamilisha juhudi za wiki kadhaa za kuwaondoa nchini humo.

Waandishi hao, ni miongoni mwa raia wa kigeni waliokuwa wamekwama nchini Afghanistan, kufutia Marekani na washirika wake kuamua kuondoa majeshi yao, jambo lililowafanya wanamgambo wa Taliban, kurejea madarakani.

Kwa jumla kundi la watu 72 linalojumuisha waandishi tisa ikiwemo mwandishi habari pekee mwanamke wa DW nchini Afghanistan pamoja na familia zao wameondoka salama nchini humo.

Kundi la waandishi hao lilikwama kwa wiki kadhaa mjini Kabul baada ya kushindwa kusafiri kupitia uwanja wa ndege wa mji huo kutokana na mparaganyiko uliojitokeza katika siku za mwisho za kuondoka vikosi vya kigeni.

Mkurugenzi Mkuu wa DW, Peter Limbourg, amesifu hatua ya kuondolewa kwa waandishi hao nchini Afghanistan.

DW iliwataka waandishi wake wote wa habari nchini Afghanistan kwenda mjini Kabul wakati ilipokuwa wazi kwamba kundi la Taliban lilikaribia kuchukua udhibiti wa taifa hilo.

Hata hivyo, ilikuwa vigumu kuwasafirisha haraka na kundi hilo la waandishi na familia zao lilisalia kwa siku kadhaa kwenye lango la kaskazini la uwanja wa ndege mjini Kabul, sehemu ambayo kulishuhudiwa tafrani kubwa kwa wote waliokuwa wakisubiri kuingia uwanjani.

Baada ya majaribio kadhaa iliafikiwa kwamba kundi hilo litaondoka nchini humo kupitia mpaka wa Pakistan wa Torkham ulio kiasi kilometa 180 kutoka mji mkuu wa Afghanistan.

Limbourg ameitaja hatua ya kuondoka waandishi hao nchini Afghanistan kuwa mafanikio makubwa katika wakati hali ya uhuru wa habari nchini humo ikiwa ya mashaka, tangu kundi la Taliban lilipochukua madaraka.

Hali si shwari Afghanistan, na kwamba hayo yanajiri wakati mataifa ya magharibi yanaendelea kuondoa raia wake na waafghani waliokuwa washirika wake kutoka nchini humo.

Kwengineko waziri wa mambo ya kigeni wa Uhispania, Jose Manuel Albares amewasili nchini Pakistan kuomba msaada wa kufanikisha kuondolewa kwa Waafghani waliofanya kazi na vikosi vya jeshi la nchi yake.

Mwanadiplomasia huyo ameapa kuwa nchi yake itafanya kila iwezalo kuwaondoa kutoka Afghanistan wale wote waliowasaidia wanajeshi wa Uhispania na ambao wako kwenye hatari ya kulengwa na watawala wa Taliban kama njia ya kulipa kisasi.

Nchini Afghanistan kwenyewe ripoti zinasema, Taliban wanapiga doria kwenye kila pembe ya taifa hilo ikiwemo kwenye mji mkuu Kabul, kutafuta watu waliokuwa wakiwapinga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mkutano wa Quad Hiroshima waibuka na kutafuta amani na ustawi wa Indo-Pacific

Spread the love  JITIHADA za mazungumzo ya Pande Nne (Quad), hazikuthaminiwa na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Kimataifa

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini China chaongezeka

Spread the love  WAKATI kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini...

Kimataifa

Kampuni za kigeni zahofia kuendelea na biashara China

Spread the love OPERESHENI ya kiuchunguzi inayofanywa na Serikali ya China kwa...

error: Content is protected !!