January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takwimu kupima viashiria vya maendeleo

Spread the love

OFISI ya Takwimu Taifa inatarajiwa kufanya mkutano utakaokusanya wadau wa takwimu kujadili jinsi ya kupima viashiria vya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), utakaofanyika oktoba 8, 2015. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa ,Veronica Kazimoto alipozungunza na waandishi wa habari leo Jiji Dar es Salaam.

Amesema kuwa, takwimu hizo zitawezesha taifa kupima utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na mipango mengine kama mpango wa maendeleo wa Tanzania 2025 na kwamba, mkutano huo utakuwa na mijadala mahususi ya kujadili na kuhakiki takwimu za viashiria vya mpango huo.

Mkutano huo utahudhuriwa na wadau zaidi ya 100 kutoka katika Wizara, Idara, Wakala na Taasisi ambapo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Amesema kuwa, kabla ya nchi wakuu wa nchi kujadili kukuwa kwa maendeleo, kulikuwa na mpango wa malengo ya millenia ambayo nchi nyingi za Afrika ikiwemo na Tanzania hazikufika malengo yote kwa ukamilifu hivyo Ofisi ya Takwimu itakuwa sehemu ya kuchochea kasi ya kutimiza malengo hayo.

Aidha malengo hayo yalifikiwa nchini Marekani baada ya wakuu wa nchi mbalimbali kujadili Mpango Mpya wa Maendeleo Endelevu wenye malengo 17 (SDGs) kufuatiwa kumalizika kwa Malengo ya Mellenia (MDGs) ambao utekelezaji wake ulikuwa kwa miaka 15 (2000- 2015). Mpango huu mpya utaanza mwaka huu hadi 2030.

error: Content is protected !!