Tuesday , 27 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Takukuru yawadaka tisa akiwemo mtia nia Arusha CCM
Habari Mchanganyiko

Takukuru yawadaka tisa akiwemo mtia nia Arusha CCM

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inawashikilia watu tisa wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kwa makosa mbalimbali ya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea)

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, James Ruge leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 imesema, miongoni mwa waliokamatwa ni Lilian Ntiro, mtia nia wa kugombea ubunge viti maalum mkoani Arusha kupitia kundi la wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wengine ni; Sifael Siyaloi Pallangyo, Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkoani Arusha. Upendo Malulu Ndoros, Katibu wa Malezi wilayani Longido na mjumbe wa Baraza la Wazazi mkoa wa Arusha.

Pia wamo, Laraposho Katewa Laizer, Katibu wa Wazazi Wilaya ya Longido, mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa wa Arusha. na Godwait Charlse Mungure, Katibu wa Wazazi Kata ya Kikatili Meru.

Ruge amesema, mtia nia huyo alimpatia fedha Sifael Pallangyo, ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi Arusha za kuwahonga wajumbe wa baraza hilo, ili kuwashawishi wamchague kuwa mbunge viti maalum.

Amesema walibaini sakata hilo, baada ya kupewa taarifa kutoka kwa raia mwema, tarehe 26 Juni 2020.

Amesema baada ya Takukuru kupata taarifa hizo, iliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, huku kila mmoja akiwa na kiasi tofauti cha fedha, zilizokuwa zimeandaliwa kugawiwa kwa wjaumbe wa baraza hilo.

“Ntiro ambaye anatarajiwa kugombea ubunge viti maalumu kundi la wazazi mkoani Arusha, alikuwa amempatia Pallangyo fedha, kwa ajili ya kwenda kuwahonga wajumbe wa baraza la wazazi katika Wilaya ya Longido, kama kishawihsi cha kumpigia kura katika kura za maoni zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni,” amesema Ruge.

Ruge amesema Sifael Pallangyo alikutwa na Sh. 14,000, wakati Malulu alikamatwa akiwa na Sh. 552,000 pamoja na simu aina ya Itel smart phone, ambayo ilikuwa na mawasiliano baina yake na watuhumiwa wenzake katika sakata hilo.

Laizer alikutwa na Sh. 117,000 pamoja na simu aina ya Samsung Galax ambapo pia kulikuwa na mawasiliano na watuhumiwa wenzake. Mungure alikutwa na simu ndogo yenye mawasiliano ya mara kwa mara na Pallangyo.

Ruge amesema, uchunguzi wa sakata hilo unaendelea na watuhumiwa wako mahabusu tangu tarehe 26 Juni 2020, huku baadhi yao wanatarajia kupewa dhamana leo.

“Takukuru inaendelea kumshikilia mtia nia Lilian Ntiro kwa mahojiano zaidi,” amesema Ruge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

Habari Mchanganyiko

Oryx wagawa mitungi 1000 kwa viongozi wa dini, wajasiriamali Moshi

Spread the loveVIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali pamoja na wajasiriamali katika...

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!