Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco
Habari Mchanganyiko

Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru
Spread the love

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imerejesha vifaa ghafi vya umeme vyenye thamani ya zaidi Sh. 420 milioni kwa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Vifaa hivyo vilivyokuwa vikishikiliwa na wakandarasi wanne, ambapo waliokuwa wakitekeleza Awamu ya Pili ya Mradi wa Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Mawakala hao ni Derm Electrics (T) Ltd, M/S JV States Grid Electrical & Technical Works Ltd. Nakuroi Investments na Urban and Rural Engineering Services Ltd.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 27 Februari 2021, na Mkurugenzi Mkuu Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa Naibu Mkurugenzi Tanesco, Mhandisi  Isaack Chanji, kwenye ofisi za shirika hilo, Tawi la Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Brigedia Mbungo amesema, vifaa hivyo vimerudishwa baada ya agizo lake alilolitoa mkoani Iringa mwishoni mwa 2020, lililowataka wakandarasi waliokuwa wakidaiwa na serikali vifaa, kuvirejesha ndani ya siku 14.

“Katika kutekeleza agizo hili, baadhi ya Wakandarasi walifika katika ofisi za Takukuru kuhakiki na kutambua aina na idadi ya vifaa ghafi vya umeme wanavyotakiwa kuvirejesha TANESCO,” amesema Brigedia Mbungo.

Vifaa vilivyorejeshwa Tanesco na Takukuru ni mashine za usambazaji umeme (Transfoma) 30 zenye ukubwa tofauti tofauti pamoja na taa za umeme za matumizi madogo ya umeme (Energy Saver Bulbs) 20,000.

Mkuu huyo wa Takukuru amesema taasisi hiyo iliamua kuingilia kati sakata hilo, kwa kuwa wakandarasi hao walipaswa kuvirudisha tangu 2017.

“Vifaa hivi vilitakiwa viwe vimerejeshwa TANESCO  2017 na Mkandarasi M/S JV States Grid Electrical & Technical Works Ltd, ambaye alitekeleza Mradi wa REA II Mkoani Kigoma na kuukamilisha tangu mwaka 2017,” amesema Brigedia .

Aidha, Brigedia Mbungo amesema kuna baadhi ya wakandarasi wamewasilisha taarifa zao za miradi  Takukuru, kwa ajili ya kuhakikiwa ili warudishe vifaa ghafi.

“Vilevile, wapo baadhi ya Wakandarasi ambao tayari wamewasilisha taarifa zao za miradi ili zihakikiwe na TAKUKURU tayari kwa kuanza zoezi la kurejesha vifaa ghafi,” amesema Brigedia Mbungo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!