Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Takukuru yapangua safu ya viongozi Arusha
Habari Mchanganyiko

Takukuru yapangua safu ya viongozi Arusha

Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani
Spread the love

BRIGEDIA Jenerali John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), amepangua vituo vya kazi vya maafisa sita wa taasisi hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo Jumamosi tarehe 27 Juni 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru.

Taarifa ya Doreen inaeleza, watumishi watano kati ya sita waliobadilishiwa vituo vya kazi, walikuwa katika vituo vya kazi vilivyoko jijini Arusha.

Pangua pangua hiyo imemgusa Frida Wikesi, aliyekuwa Mkuu wa Takukuru mkoani Arusha, ambaye amerudishwa makao makuu ya taasisi hiyo katika kitengo cha kurugenzi ya uchunguzi.

James Ruge, aliyekuwa Afisa Uchunguzi katika Ofisi Mkurugenzi Mkuu Takukuru makao makuu, ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Arusha.

Jonathan Shana, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Arusha

Zawadi Ngailo, aliyekuwa Mkuu wa Takukuru, Wilaya ya Arumeru, amehamishiwa Ofisi ya Takukuru mkoa wa Arusha. Wakati Deogratius Peter, aliyekuwa Mkuu wa Takukuru wa Wilaya ya Siha, akihamishiwa Wilaya ya Arumeru.

Katika mabadiliko hayo, David Shirima, aliyekuwa Mkuu wa Takukuru wilayani Monduli, amekuwa Mkuu wa Takukuru wilayani Siha.

Pia, Mariam Mayaya, aliyekuwa Afisa Uchunguzi Mkuu Takukuru Mkoa wa Arusha, amebadilishwa kuwa Mkuu wa Takukuru wilayani Monduli.

Doreen amesema mabadiliko hayo ni ya kawaida ili kuimarisha utendaji kazi wa ndani wa Takukuru.

“Juni 22, 2020 Brigedia Mbungo amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya viongozi na watumishi. Uhamisho huu ni wa kawaida umefanyika ili kuimarisha utendaji kazi ndani ya Takukuru,” inaeleza taarifa ya Doreen.

Mabadiliko hayo yamekuja siku kadhaa baada ya Rais John Magufuli tarehe 22 Juni 2020, wakati akiwaapisha viongozi wapya wa mkoa wa Arusha aliowateua, alitoa onyo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Jonathan Shana na Mkuu wa Takukuru mkoa huo, Wikesi.

Rais Magufuli alisema viongozi hao wamekuwa hawafanyi yale aliyowatuma na kujiingia kwenye kazi ambazo si za kwao.

Rais Magufuli alitoa onyo hilo wakati akimwapisha Iddi Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi Mrisha Gambo ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi wa TAKUKURU

Baada ya onyo hilo, tarehe 24 Juni 2020, IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alimhamisha Shana kuwa Afisa Mnadhimu namba moja wa Shule ya Polisi Moshi.

Katika mabadiliko hayo, IGP Sirro alimteua Salum Hamduni, kuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Arusha na leo tarehe 27 Juni 2020, Brigedia Mbungo ametangaza kumhamisha Wikesi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!