July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yaokoa Mil 14.4

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Morogoro imeeleza kuokoa Sh. 14.4 milioni baada ya kufanya ukaguzi kwenye miradi 16 yenye thamani ya Sh. 3 bilioni, anaandika Christina Haule.

Taasisi hiyo imeeleza kubaini baadhi ya watendaji kwenye miradi hiyo kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika matumizi ya fedha za serikali katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

Emmanuel Kiyabo, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Morogoro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi kuhusu taarifa ya miezi mitatu ya taasisi hiyo mjini humo.

Amesema kuwa, katika uchunguzi huo wa fedha za miradi wamefanikiwa kuokoa kiasi hicho cha fedha ambazo zilikuwa mikononi mwa baadhi ya watuhumiwa ambapo sasa zimeingizwa kwenye akaunti maalum ya serikali ya fedha zinazookolewa.

Hata hivyo amesema, Takukuru katika kipindi hicho pia imefanikiwa kuokoa Sh. 13.2 Mil ikiwa ni gharama ya kuweka alama za barabarani katika Manispaa ya Morogoro ambapo mkandarasi alilipwa bila kufanya kazi hio katika barabara za Kitope, Kingo, Mlapakolo na Nguzo na kwamba, kazi hiyo ilifanyika baada ya uchunguzi kuanzishwa na Takukuru.

error: Content is protected !!