May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yamwachia ‘bosi’ bandari, “waulizwe CAG”

Desdedit Kakoko, aliyekuwa Mkurugezi wa mamlaka ya Bandari

Spread the love

 

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema, imemwachia kwa dhamana, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya kushikiliwa kwa siku kadhaa na Takukuru, siku chache kupita, tangu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutangaza kumsimamisha kazi, kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh.3 bilioni ndani ya mamlaka hiyo.

Rais Samia alitoa maagizo hayo, Jumapili ya tarehe 28 Machi 2021, mara baada ya kupokea ripoti mbili za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ya Takukuru zote za mwaka 2019/20, Ikulu ya Chamwoni, mkoani Dodoma.

Mara baada ya maagizo hayo, Kakoko ilimkamata kwa mahojiano ambapo leo Jumamosi, tarehe 17 Aprili 2021, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo akijibu swali la MwanaHALISI Online, lililotaka kujua kinachoendelea ambapo amesema “tumemwachia kwa dhamana.”

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru

Mbungo amesema, “uchunguzi wenye tuhuma kubwa kama hii, unahusisha watu wengi sana na akikosekana hata mmoja, unaweza usikamilike. Lakini sisi (Takukuru), tumekamilisha kwa asilimia 98 na asilimia mbili zimebaki kwa CAG.”

Amesema, CAG anafanya ukaguzi wa athari iliyotokana na ubadhirifu huo kisha apelekewe Mwendesha Mashataka wa Serikali (DPP), ambaye naye atapeleke jalada hilo mahakamani.

“CAG lazima aandae uchunguzi maalum wa hasara iliyopatikana na sisi tunaweza kuwa tumekamilisha, lakini CAG kama hajamaliza hawezi kupeleka kwa DPP na DPP hawezi kuupeleka mahakamani,” amesema Mbungo

Bosi huyo wa Takukuru amesema “Takukuru imekamilisha asilimia 98 na asilimia mbili niya CAG ya ukaguzi maalum. Sasa waulizeni CAG kuwa ukaguzi huo maalum mmekwisha ukamilisha? Na ukienda kwa DPP, mnamuuliza DPP, lini litakwenda mahakamani?

MwanaHALISI Online, limeutafuta uongozi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujua ukaguzi huo maalum ulipofikia, bila mafanikio. Jitihada zaidi zinaendelea kuutafuta, akiwemo CAG mwenyewe, Charles Kichere.

error: Content is protected !!