May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yamshikilia Mfanyabiashara Dodoma

Brigedia Jenerali, John Mbungo

Spread the love

TAALIB Karim Mbowe, mfanyabiashara na mmiliki wa Kampuni ya White Star Investiment jijini Dodoma anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma tatu ikiwemo kukwepa kodi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya Takukuru leo tarehe 16 Agosti 2020, Mbowe anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi, udanyanyifu na utakatishaji fedha haramu.

Mbowe kupitia kampuni hiyo, ni wafanyabiashara ya usafirishaji ndani nan je ya nchi kwa kutumia malori.

Kwenye taarifa hiyo iliyosainiwa na Doreen Kapwani, Ofisa Uhusiano wa Takukuru kwa niaba ya Brigedia Jenerali John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Takukuru inaendelea kuchunguza umiliki wa vichwa vya malori (Treller) zaidi ya 100 vinazomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

Taasisi hiyo pia inachunguza mikopo yake ya Dola za Marekani zaidi ya 3,000,000 kutoka Benki ya Barclays na dola 540,000 kutoka katika Benki ya Equity.

error: Content is protected !!