May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yamkamata kigogo bandari akiwa mafichoni

Frank Mkilanya, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza

Spread the love

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imemkamata aliyekuwa Mhasibu wa Mamlaka ya Bandari Kigoma, Madaraka Robert Madaraka anayetuhumiwa rushwa, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi wa Sh.153.5 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Madaraka ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa waliokuwa watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkoa wa Kigoma, amekamatwa akiwa mafichoni katika eneo la Nyasaka Wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza.

Taarifa ya kukamatwa kwa Madaraka, imetolewa leo Jumanne, tarehe 20 Aprili 2021 na Frank Mkilanya, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza.

Mkilanya amesema, mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa na Takukuru tangu Agosti,
2020 ili aweze kuunganishwa na wenzake watano ambao walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma tangu tarehe 31, Agosti 2020.

Amewataja washtakiwa hao watano ni; Rodrick Ndeonasia Uiso- Mkurugenzi wa Kampuni ya Saxon Building Contractors Limited, Ajuaye Kheri Msese -aliyekuwa Meneja wa Bandari Kigoma, Herman Ndiboto Shimbe- aliyekuwa Afisa Uhasibu TPA Kigoma, Jesse Godwin Mpenzile – aliyekuwa Mhandisi Mkazi TPA Kigoma na Lusubilo Anosisye Mwakyusa -Aliyekuwa Afisa Rasilimali watu TPA Kigoma.

error: Content is protected !!