August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yalia na rushwa Mahakama ya Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imelalamikiwa kuwa inaendekeza vitendo vya rushwa katika utoaji haki, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza baada ya kuachiliwa huru Williamu Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Leornaed Swai Mwanasheria wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) amesema kuwa rushwa katika mahakama ya Kisutu inatisha.

Swai ametoa tuhuma hizo baada ya Hakim Hellen Liwa kusoma hukumu kwa niaba ya Kwey Rusema ambapo iliamriwa kuwa mahakama imemuona Mhando hana hatia.

Mahakamaa imeeleza kuwa hakuna ushahidi ilionyesha kuwa Mhando alitumia madaraka yake vibaya kutokana na mkataba wa Tanesco kuipa zabuni ya mkewe kampuni ya Santa Clara, na pia yeye hakuhusika kwenye kutoa zabuni kwa kuwa zabuni hutelewa na bodi ya zabuni.

Mahakama imeeleza kuwa hakuna ushahidi wa yeye kujua kuwa Santa Clara ni kampuni ya mke na watoto wake kwani inwezekana mke akawa na akaunti benki mumewe asijue.

Mshtakiwa namba mbili Eva Mhando ameonekana hana hatia kutokana na hakuna ushahidi ulionyesha kuwa ameghushi nyaraka.

Kesi ilikvyokuwa

Mhando na mkewe walikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia Sh. Milioni 31.7 kwa njia ya udanganyifu.

Kadhalika, Mhando alikabiliwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd, huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.

Mwendesha Mashitaka wa Taasisi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliwasomea mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi na kwamba washitakiwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 31, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco jijini Dar es Salaam, Mhando akiwa kama Mkurugenzi wa shirika hilo, alitumia vibaya mdaraka yake kwa kujiingizia maslahi yake binafsi

Mshitakiwa aliipa zabuni kampuni inayongozwa mke wake, Eva na watoto wake, ya kusambaza vifaa vya Tanesco vyenye thamani ya Sh. Milioni 884.5 na kuisababishia kampuni hiyo kupata faida ya Sh. 31,747,000 kinyume cha sheria .

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 6 na Julai 30, 2011, mahali pasipofahamika, jijini Dar es Salaam, Eva alighushi taarifa ya ukaguzi wa fedha ya Kampuni ya Santa Clara Ltd, akionyesha kwamba imekaguliwa na Finx Capital House Desemba mwaka 2010.

Katika shitaka la tatu, 9Agosti, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Eva alighushi nyaraka za umiliki wa hisa kutoka Santa Clara Supplies Ltd kwenda Eveta John Shing’oma huku akijua siyo kweli.

Shitaka la nne, 5 Agosti, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco, jijini, mshtakiwa Eva aliwasilisha nyaraka za manunuzi za kughushi akionyesha kwamba taarifa hiyo imeandaliwa na Finx Capital House huku akijua siyo kweli.

Katika shitaka la tano, ilidaiwa kuwa kati ya Aprili na Oktoba, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, Eva akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Santa Clara Limited kwa nia ovu, alijipatia faida ya Sh. 31.7 milioni  kutoka Tanesco baada ya kuwasilisha nyaraka za ukaguzi za kughushi.

Shitaka la sita, 17 Oktoba , mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco, mshtakiwa wa tatu hadi wa tano, Mchalange, Misidai na Kisinga wakiwa watumishi wa shirika hilo, walipokea nyaraka za kughushi na kusababisha Kampuni ya Santa Clara Supplies Limited kupewa mkataba wa kusambaza vifaa vya ofisini. Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulisababisha kampuni hiyo kupata mkataba wa zabuni ya kusambaza vifaa vya Sh. 884.5 milioni na kupata faida ya Sh. 31.5 milioni.

error: Content is protected !!