April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yaingilia kati mradi wa maji Chemba

Sisthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Dodoma imeingilia kati ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kiniji cha Kelema Kuu, wilayani Chemba baada ya kubaini thamani ya fedha iliyotumika kutoendana na kazi halisi iliyofanyika. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Sisthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma akitoa taarifa ya robo mwaka kwa waandishi wa habari amesema, hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni moja ya majukumu ya taasisi hiyo chini ya kifungu cha 7 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.

Kibwengo amesema kuwa, katika uchunguzi wao wamebaini kwamba, thamani ya fedha haikupatikana kutokana na uwepo wa malipo zidifu ya kazi halisi zilizofanyika na kutandikwa kwa aina ya mabomba kinyume na mkataba hivyo kusababisha mradi huo kutotoa maji.

“Baada ya Takukuru kuingilia kati mkandarasi wa mradi huo Juin Company Limited, ameridhia kurekebisha mapungufu yaliyobainika na leo Julai Mosi mwaka huu, anaanza kazi ya kubadili mabomba na kuweka yanayostahili.

“Sambamba na hilo mkandarasi amekubali kurejesha fedha zidifu aliyolipwa bila kustahili, hivyo jumla ya Sh. 67,542,600 zimeokolewa na ni matarajio kuwa wananchi watapata huduma ya maji,” amesema.

Ameeleza kuwa, mradi huo huo wenye thamani ya Sh. 222,978,680 ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2015.

Katika hatua nyingine Kibwengo amesema kuwa, wamefanikiwa kumkamata Mkurugenzi wa Global Space East Afrika Limited, Gaston Francis.

Amesema kuwa, mkurugenzi huyo alipewa kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mima Wilaya ya Mpwapwa ambaye alitangazwa kutafutwa Aprili Mosi mwaka huu.

Na kuwa, baada ya uchunguzi, wamebaini kuwa kampuni hiyo imelipwa isivyo halali kiasi cha Sh. 86,405,205 kwa kazi ambazo hazikufanyika .

Pia Kibwengo amesema kuwa, Takukuru imeokoa na kurejesha serikalini jumla ya Sh. 11, 877, 353.

error: Content is protected !!