April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TAKUKURU wamwachia Nyalandu, Polisi wamnyima dhamana

Spread the love

JESHI la Polisi Singida Mjini limemnyika dhamana Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Kaskazini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na wenzake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Nyalandu leo mapema alishikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Singida kwa mahojiano pamoja na David Jumbe na Samson ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, Kata ya Itaja.

Kwa mujihu wa taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene, Afisa Habari wa Chadema, inasema baada ya mahojiano TAKUKURU walimua kuwaachia Nyalandu na wenzake lakini Jeshi la Polisi waliwashikiria kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya Polisi kumaliza kuwahoji na kuandikisha maelezo waliruhusiwa kwa dhamana, lakini ghafla OCD akabadili uamuzi akidai amepokea maelekezo.

error: Content is protected !!