March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru waingia kazini ‘issue’ ya Nyalandu

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema kuwa suala la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imelisikia na imeanza kulifanyia kazi, anaandika Angel Willium.

Takukuru wameingia kazini kulifanyia kazi shutuma za Nyalandu baada ya kutuhumiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, alipokuwa anachangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018 na kuiagiza taasisi hiyo na polisi kumchunguza Nyalandu.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema wamesikia tuhuma za Nyalandu na wameanza kuzichunguza na wakimkuta na hatia watamfikisha kunakostahili.

Mbugo ameitoa kauli hiyo leo ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Dk. Kigwangala kumlipua Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Dk. Kigwangala amesema Nyalandu aliikosesha serikali mapato ya Sh. 32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

error: Content is protected !!