August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TAKUKURU Temeke yapokea malalamiko 29 ya rushwa

Spread the love

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Temeke imepokea malalamiko 29 yanayohusisha vitendo vya rushwa kutoka katika maeneo tisa tofauti. Anaripoti Erick Mbawala (TURDACO) … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumatano tarehe 3 Agosti, 2022, katika taarifa ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Temeke, Holle Makungu kuhusu uutekelezaji wa wa majukumu yake katika robo ya Aprili hadi Juni, 2022.

Maeneo yaliyolalamikiwa na idadi ya malalamiko kwenye mabano ni Tamisemi (7), ardhi (4), binafsi (6), Access Bank(01), Mahakama(03), afya(02), elimu(01), polisi(02) na zinazohusu siasa (02).

Aidha Makungu amesema taarifa 18 kati ya hizo tayari zimeshughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na kufunguliwa majalada ya uchunguzi na uchunguzi unaendelea.

“Kati ya kesi 11 za Rushwa, mbili zimehamishiwa idara nyingine za uchunguzi na tisa zilizobaki walishauriwa mahali pa kuzipeleka, kesi mbili zimefunguliwa katika mahakama ya Temeke na Kigamboni na kufanya kesi zinazoendelea mahakamani kuwa 14,” amesema Makungu.

TAKUKURU Temeke imeahidi kuendelea kutoa elimu juu ya rushwa na kufuatilia miradi ambayo inapaswa ikamilike kwa wakati na matumizi ya bajeti ambazo zinapaswa kutumika katika miradi hiyo.

Makungu amesema wana mkakati wa kuendelea kufuatilia makusanyo na uwasilishaji wa mapato yanayotokana na mashine za POS na kuchukua hatua kwa watakaofuja mali za umma, kwa lengo la kukomesha maswala ya rushwa katika mkoa huo.

error: Content is protected !!