
TAASISI ya Kuzuzia na Kupambana na Rushwa Tazania (Takukuru), imeingia makataba na Serikali ya Palestina kupambana na rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Makubaliano hayo yamefikiwa leo Alhamisi tarehe 11 Februari 2021, katika ofizi ya Takukuru Dar es Salaam ambapo Palestina imewakilishwa na balozi wake, Hamdi Mansour AbuAli huku Tanzania ikiwakilishwa na mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo, Brigedia Jenerali, John Julius Mbungo.
Nchi hizo mbili zimeeleza, suala la kukabiliana na rushwa ni juhudi zinazopaswa kufanywa na nchi zote mbili, na kwamba zimekubaliana kubadilishana uzoefu na mbinu mbalimbali.
“Suala la rushwa si janga la ndani ya nchi tu, bali limekuwa janga la kimataifa na huathiri uchumi wa nchi na maelewano ya jamii,” amesema Balozi AbuAli.
Wawili hao wamekubaliana kuimarisha juhudi na kubadilishana uzoefu kwa kuzingatia n misingi na masharti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya rushwa.
Pia, kwa kuzingatia mkataba wa Umoja wa Afrika, Mkataba wa Kiarabu dhidi ya rushwa na kanuni za urafiki na masilahi ya pamoja.
More Stories
Waziri Mulamula ashiriki mkutano wa Baraza la Mawaziri AU
Walimu Sekondari ya Aga Khan wagoma kisa ubaguzi wa rangi
NMB yatenga bilioni 1 kusaidia wabunifu wachanga, Waziri apongeza