Wednesday , 6 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Takukuru msimsubiri DPP, nendeni kortini – JPM
Habari za Siasa

Takukuru msimsubiri DPP, nendeni kortini – JPM

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imetakiwa kutumia mamlaka yake, kuwafungulia kesi mahakamani watuhumiwa wa makosa ya rushwa, bila kusubiri kibali kutoka kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano tarehe 22 Julai 2020 na Rais John Magufuli, wakati akizindua Ofisi za Takukuru Wilaya ya Chamwino, zilizoko maeneo ya Chikuyu B, jijini Dodoma.

Rais Magufuli ameishauri Takukuru kuwafikisha mahakamani moja moja kwa watuhumiwa, wenye tuhuma zisizo na ulazima wa kuthibitishwa na ofisi ya DDP, kwa kuwa ofisi hiyo ya mashtaka ina majukumu mengi.

“Kila kesi mnasubiri kibali cha DPP, ofisi ya DPP nayo ina makesi mengi wakati mwingine mnapeleka ushahidi haupo, anawarudishia jalada haoni mahali kesi itasomwa, niwaombe wakubwa wa Takukuru yale mnayoweze kushirikiana ninyi bila ya DPP mshughulikie,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema “Msitafute kisingizio cha kutopeleka mahakamni sababu ya DPP, yapo yanayotakiwa kwenda DPP, yapo mengine wala hayahitaji.”

Rais John Magufuli

Rais Magufuli ameitaka Takukuru kutumia vifungu vya sheria, vinavyoipa mamlaka ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani moja kwa moja, pasina kibali cha ofisi ya Takukuru.

“Lakini mnakifungu cha sheria nafikiri cha 15, kinawapa mamlaka kupeleka mahakamani moja kwa moja, kwa nini hamkitumii hiki kifungu mpaka mnasubiri kibali cha DPP?” amehoji Rais Magufuli.

Kiongozi huyo wa nchi amesema kuna majalada mengi yanachelewa kufikishwa mahakamani, kutokana na Takukuru kurushiana mpira na ofisi ya DPP.

“Yapo mambo yanachelewa kwa sababu ya kusingiziana Takukuru na ofisi ya DPP, kwamba hii kesi haijapelekwa mahakami ofisi ya DPP haijatoa kibali,” amesema Rais Magufuli.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, ameitaka Takukuru kuwafuatilia wagombea wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020. Ili kudhibiti vitndo vya rushwa.

“Takukuru mnang’ata kweli lakini kuna mahali mnang’atwa ng’atwa kidogo, mfano kwenye chaguzi hizi kuna watu mlitumika kuharasi. Kwa wenye majimbo yao Takukuru wako nyuma lakini wakiingia wazengeaji mnatulia, kuna vitu vidogo vidogo kama hivyo naomba mjirekebishe,” amesema Mama Samia.

Spika Job Ndugai, ameitaka Takukuru kufuatilia kw aukaribu michakato ya uchaguzi ndani ya vyama vya siasa.

“Takukuru mmetusaidia si kama miaka mingin, mmesaidia kuweka hali ya hewa vizuri, mfanye hivyo kwa vyama vyote na hasa kwenye uchaguzi mkuu mng’ate zaidi,” amesema Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!