April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TAKUKURU: Lugola na wenzake wana kosa la uhujumu uchumi

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jenerali John Mbungo

Spread the love

KUMEBAINIKA makosa mengi ya kijinai katika mkataba wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto ambao ulisababisha Rais Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi watendaji akiwemo Kangi Lugola aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Anaandika Regina Mkonde (endelea).

Makosa hayo yaliyothibitika kutokana na uchunguzi ulioendeshwa na taasisi hiyo mara baada ya rais kufichua ufisadi huo kwenye mkutano, kwa pamoja yanatengeneza kosa la kisheria la uhujumu uchumi.

Hayo ndiyo maelezo yaliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo alipokutana na waandishi wa habari jijini.

Brigedia Jenerali Mbungo amesema kufuatia ugunduzi huo katika uchunguzi ulioelekezwa na Rais Magufuli, sasa atawasilisha matokeo yake kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuandaa mashitaka dhidi ya Lugola na wenzake 16.

Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema uchunguzi umebaini makosa ya wazi kwenye mkataba huo ambao Rais Magufuli aliueleza kuwa umeendelea kuonesha kuwa watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani si waadilifu.

Alisema wizara hiyo imekuwa ikimtesa tangu alipoingia madarakani Novemba 2015 na ameshangaa watendaji hao hawajabadilika pamoja na kujua kuwa yeye amekuwa mkali kwa mafisadi na wabadhirifu wa mali ya umma.

Siku hiyo alisikika akisema kuwa ameshangaa kukuta Lugola amehudhuria hafla ile wakati ameshindwa kuchukulia hatua watendaji walio chini yake, tofauti na Katibu Mkuu Milanzi aliyekuwa tayari ameandika barua ya kujiuzulu.

Rais Magufuli hapohapo alisema alikuwa ameridhia barua ya Lugola kuomba kujiuzulu na kwamba TAKUKURU ianzishe uchunguzi mara moja.

Alisema hana urafiki na watenda ufisadi na kwamba anachukua hatua pamoja na kuwa Lugola ni mwanafunzi wake.

Mbali na Lugola ambaye ni mbunge wa jimbo la Mwibara, mkoani Mara, wengine waliotimuliwa kuhusu sakata hilo ni Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye, aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi.

 

error: Content is protected !!