April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru kufuatilia kwa karibu Uchaguzi Serikali za Mitaa

Sanduku la kura

Spread the love

UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, utafuatiliwa kwa karibu zaidi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU). Anaripoti Regina Moonde … (endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 28 Machi 2019 na Kamishna Diwani Athuman, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru wakati akimkabidhi Rais John Magufuli taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo katika mwaka wa fedha wa 2017/18, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kamishna Diwani amesema, Takukuru imejipanga vizuri kuzuia na kupambana na rushwa kabla na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

 “Tumeanza ufuatiliaji wa rushwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tumejipanga kuzuia vitendo vya rushwa kabala na baada ya uchaguzi.

“Miongoni mwa mikakati yetu ya kushughulikia hilo, Takukuru imeandaa warsha mbalimbali kwa lengo la kukutana na wadau husika ili kujadili katika kuhakikisha tunadhibiti vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi,” amesema Kamishna Diwani.

Aidha, Kamishna Diwani amesema taasisi yake imebaini ufisadi katika miradi 63 yenye thamani ya zaidi ya Sh.  62 bilioni.

Na kwamba, walibaini ubadhirifu huo katika ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma kwenye miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha wa 2017/18.

Amesema katika ukaguzi wa miradi hiyo, walibaini ufujaji wa fedha za umma, ikiwemo kutumika kwa vifaa vilivyo chini ya kiwango ikilinganishwa na fedha halisi zilizopangwa katika bajeti ya miradi hiyo.

 “Takukuru jukumu letu ni kufuatilia fedha za umma katika miradi ya maendeleo, kwa mwaka 2017/18 tulikagua miradi 661 yenye thamani ya zaidi ya trilioni 1.

“Ilibaini ufisadi katika miradi 63 yenye thamani ya 62.5 bilioni. Ufujajaji uliobainika ni matumizi ya vifaa vilivyochini ya kiwango, na 408 ilichelewa kukamilika kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Katika hatua nyingine, Kamishna Diwani ameeleza mafanikio ya taasisi yake katika kupambana na rushwa katika mwaka wa fedha wa 2017/18

Na kuwa, imefanikia kutekeleza malengo ya kiutendaji  kwa asilimia 81.4, kuokoa fedha za umma zaidi ya 70 bilioni ukilinganisha na kiasi cha Sh. 14.6 bilioni zilizookolewa kwa mwaka 2016/17.

“Tumeongeza idadi ya ufunguaji kesi, takribani 495 zilifunguliwa kwa mwaka 2017/18 ukilinganisha na kesi 435 zilziofunguliwa mwaka 2016/17.

“Kuhusu uchunguzi na mashtaka , majalada 906 yalifunguliwa ambapo 699 kati ya hayo yalihusu  makosa ya hongo huku  208 yakihusu makosa ya vifungu vingine vya sheria ya rushwa. Kwa ujumla kesi 624 zilienda katika mahakama, 296 zilizotolewa uamuzi na 118 waliachiwa huru,” amesema.

error: Content is protected !!