September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru Dodoma yala sahani moja  wenye madeni sugu

Spread the love

TAASISI ya Kuzuiya na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma, imevikabidhi vyama vya akiba na mikopo (Saccos) vya MWASHITA  na  DUWASA kiasi cha Sh. 74.2 milioni kutoka kwa wadaiwa  wa muda mrefu wa vyama hivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

Kupitia taarifa ya Sosthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa  Dodoma  kwa vyombo vya habari aliyeitoa leo Ijumaa tarehe 26 Juni 2020 iliyoeleza fedha hizo zilikuwa mikononi mwa wanachama 32 wa vyama hivyo jijni humo.

Kibwengo amesema,  Takukuru imeukibadhi uongozi wa mkoa Dodoma Sh. 9.3 milioni zilizookolewa kwenye vitambulisho vya wajasiriamali.

Pia, taasisi hiyo imemrejeshea kiasi cha Sh. 10 milioni Frida Nahamani  kutoka kwa Maswe Mgaya mmiliki wa Swahili Trust Microfinance .

Frida alikopa kwenye taasisi hiyio ya kifedha kiasi cha Sh. 15 milioni na kukabidhi kadi yake ya benki kwa kuwa Frida alikuwa mbioni kupata fedha zake za kustaafu aliporejesha fedha alizokuwa akidaiwa alikuta amekatwa zaidi Sh. 10 milioni.

“Uchunguzi wetu tuliuanzisha baada ya kupokea malalamiko ya Nahamani ambaye ni muuguzi mstaafu, ameonesha kati ya Julai na Desemba 2018, alikopa kiasi cha Sh. 15 milioni na akakabidhi kadi yake ya benki kwa taasisi hiyo ili warejeshe fedha zao atakapopata mafao yake”

Kibwenge amesema, Takukuru imefanya uchunguzi  kwenye mradi wa maji wa  kijiji cha Songambele  ulikiuka taratibu za manunuzi  kwenye mradi huo.

error: Content is protected !!