January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taifa Stars yajiweka mtegoni mwa Mambas, AFCON

Kikosi cha Taifa Stars

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars

Spread the love

TANZANIA, Taifa Stars imeanza vibaya hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 zitakazofanyika nchini Morocco, baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Msumbiji ‘Mambas’.

Katika mchezo huo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo, mabao ya Stars inayofundishwa na Mholanzi Mart Nooij yalifungwa na kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa.

Kwa Matokeo hayo Stars itahitaji ushindi katika mchezo wake wa marudiano utakaochezwa mjini Maputo kati ya Agosti 1 na 3 mwana huu, au sare ya mabao 3-3 ili iweze kusonga kupangwa katika kundi F kujiunga na timu za Zambia, Carpe Verde na Niger.

Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila bao na kipindi cha pili, Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 47 kwa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Elias Pelembe baada ya Kevin Yondan kucheza rafu kwenye eneo la hatari. Mcha aliisawazishia Stars bao hilo dakika ya 65 akimalizia kazi nzuri ya Thomas Ulimwengu.

Mcha tena akaifungia Stars bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 71 kwa penalti, baada ya mabeki wa Mambas kumchezea rafu Mbwana Samatta kwenye eneo la hatari.

Stars iliongeza mashambulizi langoni mwa Msumbiji na kukosa mabao kadhaa ya wazi. Msumbiji walizinduka na kufanya shambulizi zuri lililowapatia bao la kusawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho aliyetokea benchi pia.

error: Content is protected !!